MCHUNGAJI ALIYEAHIDI AKIFA ATAFUFUKA BADO YUPO MOCHWARI ZAIDI YA SIKU 400 SASA


Mchungaji maarufu kutokea Afrika Kusini ambaye alifariki dunia mwezi Agosti 2021, mpaka hii leo bado yupo ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti kilichopo katika Jimbo la Gauteng, Johannesburg nchini humo baada ya kushindwa kufufuka kama alivyoahidi.


Siva Moodley ana kundi la Wafuasi ndani na nje ya Afrika Kusini na anaheshimika miongoni mwa jumuiya ya kidini kwasababu ya ‘miujiza’ aliyoifanya wakati wa mahubiri yake pale alipokuwa hai.


Mitandao ya South Africa imeripoti kuwa tangu kifo chake karibia siku 400 zilizopita, Mchungaji Moodley amehifadhiwa kwenye nyumba ya kuhifadhia maiti iitwayo Martins Funeral Home, Taasisi hiyo, iliyoko Fourways, imelipwa ili kumweka Kiongozi huyo wa imani katika uangalizi wao lakini hata mtiririko wa pesa wa karibia R60 000 (Tsh. 8,137,595) uliotolewa kama bima ili kuhifadhi mwili huo unaanza kupungua.


Martin du Toit anayeendesha nyumba hiyo ya kuhifadhia maiti, hivi karibuni alisema anaomba idhini kutoka kwa Mahakama ili kuchoma mwili huo, huku ikionekana kuwa hata Wafusi wake wamekata tamaa juu ya ufufuo wake kwasababu mwili wake haujatembelewa na Mtu yeyote kwa zaidi ya miezi 12 sasa.


Inasemekana kuwa Mzee huyo wa miaka 53, ambaye alikuwa Mwanzilishi wa Kanisa la ‘The Miracle Centre’ lililoko kaskazini mwa jiji la Johannesburg alifariki dunia tarehe 15 Agosti mwaka jana baada ya kuugua, Kanisa lake halijakiri kifo chake kwenye mitandao yao ya kijamii mpaka leo, na akaunti zake za Twitter bado zipo active na kujibu Watu kama vile ni yeye.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments