WFP YAKABIDHI VIFAA VYA MAWASILIANO OFISI YA WAZIRI MKUU KUKABILIANA NA MAJANGA

 

Naibu  Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu ) Ummy Nderiananga.

Na Dotto Kwilasa, DODOMA

 NAIBU  Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu ) Ummy Nderiananga amepokea vifaa vya mawasiliano vitakavyotumika katika kukabiliana na maafa mbalimbali hapa nchini ambavyo ni  Ndege zisizo na Rubani (Drones) zenye thamani ya shilingi Milioni 102,741,400 vilivyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la  Mpango wa Chakula Duniani (WFP).

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Ofisi hiyo Jijini Dodoma Ummy  amesema vifaa hivyo vitawezesha Ofisi ya waziri mkuu  kutekeleza shughuli za uratibu na  udhibiti  wa maafa  mbalimbali hasa katika kuchukua taarifa  katika picha ili kupata  majanga na madhara pindi yanapotokea katika nyanja za sekta na taasisi za serikali.

Ameeleza kwamba vifaa hivyo ni muhimu kwa kuzingatia jukumu kuu la Ofisi ya Waziri Mkuu ambalo ni Uratibu wa shughuli za Serikali  na uratibu wa shughuli za maafa na taasisi zisizo za kiserikali kwa njia ya mtandao.

 “Kwa niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu, tunaishukuru WFP  binafsi na shirika la WFP kwa kutupatia vifaa hivi muhimu kwa ajili ya kuimarisha mawasiliano kwa njia ya mtandao, kufanya operesheni za utafutaji na uokoaji, kupata ramani za hatari zilizopo, uwezekano wa kuathiriwa na janga na uwezo wa jamii husika,”amesema Naibu waziri huyo.

Aidha ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na  Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kushirikiana na Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa ambayo yamekuwa yakiiunga mkono Serikali katika miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi na Taifa.

Awali akimkaribisha Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu ) Ummy Nderiananga, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. John Jingu amebainisha kwamba  Ofisi ya Waziri Mkuu iko tayari kushirikiana na  (WFP) kwa kila eneo ambalo watahitaji ushirikiano huku akiahidi vifaa hivyo kutumika kama ilivyokusudiwa.

 “Tunakumbana na maafa mengi na huwa inachukua mda mrefu kwa waokozi au upataji wa taarifa unachelewa hivyo,kwaajili ya hizi drone naamini ufanyaji kazi na upatikanaji wa uhalisia wa tukio utapatikana kwa urahisi”amesema

Aidha  Mkurugenzi Mkazi Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP)Sarah Gibson mefafanua kuwa mradi huo  ni endelevu kwa miaka mitano kuanzia Julai 2022 hadi Juni 2027 na kwamba Shirika litafanya kazi zake kulingana na vipaumbele vya serikali na kuwenkeza katika kilimo, elimu na  maafa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post