RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MWINGINE MUDA HUU


*************

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi za Mazao na Taasisi zinazosimamiwa na Wizara ya Kilimo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kama ifuatavyo:

1Amemteua Bwana Filbert Michael Mponzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT). Bwana Mponzi ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Dar es Salaam.

2)Amemteua Dkt. Tausi Mbaga Kida kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI). Dkt. Kida ni Afisa Mkurugenzi Mtendaji, Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF).

3) Amemteua Bwana Victor Kilasile Mwambalaswa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tumbaku Tanzania (TTB). Bwana Mwambalaswa ni Mbunge Mstaafu na ni Meneja Mradi wa Kampuni binafsi ya Geowind Power Tanzania Limited, Dar es Salaam.

4) Amemteua Bwana Omar Jumanne Bakari kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pembejeo wa Taifa (AGITIF). Bwana Bakari ni Mkurugenzi na Mwanzilishi Mwenza wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Tanzania Data Lab (dLab), Dar es Salaam.

5) Amemteua Bwana Salum Awadh Hagan kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB). Bwana Hagan ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya SSC Capital, Dar es Salaam.

6) Amemteua Prof. Andrew E. Temu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Afya ya Mimea na Viuatilifu (TPHPA). Prof. Temu ni Mwenyekiti wa Bodi ya Trustees of the Private Agricultural Sector Support (PASS).

7) Amemteua Bwana Abdulmajid Nsekela kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC), Bwana Nsekela ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB.

8) Amemteua Bwana Christopher Mwita Gachuma kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba Tanzania (TCB). Bwana Gachuma ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Nyanza Bottling Co. Ltd ya Jijini Mwanza.

Uteuzi wa Wenyeviti unaanza tarehe 24 Agosti, 2022.

9)Aidha, amemteua Dkt. Venance B. Mwase kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO). Kabla ya uteuzi huu Dkt. Mwase alikuwa anakaimu nafasi hiyo.



Uteuzi huu unaanzia tarehe 23 Agosti, 2022.



Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post