SIDO , NELICO & PACT WATOA MAFUNZO YA VITENDO KWA WAJASIRIAMALI MANISPAA YA SHINYANGA

Afisa Uendelezaji Biashara SIDO Mkoa wa Shinyanga, Joseph Taban (wa pili kulia) na Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga, Hopeness Eliya wakionesha sabuni zilizotengenezwa na wajasiriamali waliopatiwa mafunzo ya vitendo kwa muda wa siku 8. Aliyevaa suti nyeusi ni mgeni rasmi wakati wa kufunga mafunzo hayo, Simeo Makoba ambaye ni Meneja wa Vipindi na Mhariri Mkuu wa Redio Faraja Fm. Kulia ni Afisa Uchumi kutoka shirika la NELICO, Fortunatus Richard akifuatiwa na Afisa Uhusiano Radio Faraja, Getrude Thomas. Wa kwanza kushoto ni mmoja wa wajasiriamali hao Suzana Nuhu.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na New Light Children Center Organization (NELICO) na Shirika la PACT Tanzania wametoa mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) kwa wajasiriamali 40 kutoka kata za Ngokolo,Chamaguha, Ndala na Kambarage Manispaa ya Shinyanga kwa lengo la kuwajengea uwezo ili waweze kujiajiri na kuajiri wengine huku wakiinua uchumi wa familia na taifa kwa ujumla.

Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku 8 katika ukumbi wa SIDO Mkoa wa Shinyanga yamefungwa leo Alhamisi Agosti 18,2022 na Meneja wa Vipindi na Mhariri Mkuu wa Kituo cha Matangazo Radio Faraja Fm Stereo, Simeo Makoba.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyohusisha wanawake 39 na mwanaume mmoja, Makoba ameishukuru SIDO, NELICO na PACT Tanzania kwa kutoa mafunzo ya vitendo bure kwa wajasiriamali hao ambayo yatawasaidia kujiinua kiuchumi.

“Mmepata mafunzo haya nendeni mkatumie ujuzi mliopata kuanzisha viwanda vidogo ili mjiajiri na kuajiri wengine. Nimeo ana bidhaa mlizotengeneza ni za viwango vya hali ya juu. Kazalisheni bidhaa kwa viwango na ubunifu ili mpate masoko mazuri. Ubora wa bidhaa yako ndiyo utakuweka sokoni”,amesema Makoba.

Makoba ametumia fursa hiyo kuwataka wajasiriamali kupitia vikundi kuchangamkia mikopo inayotolewa na serikali kwenye Halmashauri za wilaya.

Aidha ameeleza kuwa hivi karibuni Radio Faraja FM Stereo itaanzisha Kipindi maalumu kwa ajili ya wajasiriamali ambapo wajasiriamali wadogo watapewa nafasi ‘Air time’ bure ya kuelezea shughuli zao.

Kwa upande wake, Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga, Hopeness Eliya amesema kazi kubwa inayofanywa na SIDO ni kutoa elimu na ujuzi kwa wajasiriamali kwa ajili ya kwenda kutengeneza bidhaa ‘Vitu halisi’ ili wajipatie kipato na kuongeza pato la taifa.

“SIDO ni walezi wa wajasiriamali, njooni SIDO mpate elimu na ujuzi wa kutengeneza bidhaa. Wajasiriamali hawa tumewapa ujuzi ‘mbegu’ ,nendeni mkaipande huko katika jamii, tunatamani kuona mnakua”,amesema Eliya.

Naye Afisa Uchumi kutoka shirika la NELICO, Fortunatus Richard amewataka washiriki wa mafunzo hayo kwenda kuwa mabalozi wazuri wa NELICO,SIDO na PACT Tanzania huku akiwasihi kutokuwa wachoyo wa ujuzi waliopata kwa watu wengine katika jamii.

“Katumieni ujuzi mliopata kujiinua kiuchumi, msiwe wachoyo wa ujuzi. Usimnyime mtu ujuzi, hata ukimfundisha hawezi kukuzidi ujuzi”,amesema.

Akisoma risala kwa niaba ya washiriki wa mafunzo,Ramadhan Hamis amesema mafunzo hayo yamewaongezea ari na hamasa ya kujiajiri ili kujipatia kipato na kwamba yatawasaidia kuzalisha bidhaa kwa tija na kuingia kwenye soko la ushindani licha ya kwamba changamoto kubwa ni mtaji na vifaa vya kufanyia kazi.

ANGALIA PICHA
Muonekano wa sabuni za maji, kufulia na kuogea, batiki na vifungashio vilivyotengenezwa  na wajasiriamali kutoka kata za Ngokolo,Chamaguha, Ndala na Kambarage Manispaa ya Shinyanga waliopatiwa mafunzo ya vitendo yaliyotolewa na SIDO, NELICO na PACT Tanzania. Picha na Kadama Malunde
Muonekano wa sabuni za kuogea ziliotengenezwa  na wajasiriamali kutoka kata za Ngokolo,Chamaguha, Ndala na Kambarage Manispaa ya Shinyanga waliopatiwa mafunzo ya vitendo yaliyotolewa na SIDO, NELICO na PACT Tanzania.
Afisa Uendelezaji Biashara SIDO Mkoa wa Shinyanga, Joseph Taban akionesha batiki zilizotengenezwa na wajasiriamali kutoka kata za Ngokolo,Chamaguha, Ndala na Kambarage Manispaa ya Shinyanga waliopatiwa mafunzo ya vitendo yaliyotolewa na SIDO, NELICO na PACT Tanzania. Kushoto ni Meneja wa Vipindi na Mhariri Mkuu wa Kituo cha Matangazo Radio Faraja Fm Stereo, Simeo Makoba akifuatiwa na Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga, Hopeness Eliya.
Meneja wa Vipindi na Mhariri Mkuu wa Kituo cha Matangazo Radio Faraja Fm Stereo, Simeo Makoba ( wa pili kushoto) akiangalia vifungashio vilivyotengenezwa na wajasiriamali waliopewa mafunzo ya vitendo na SIDO, NELICO na PACT Tanzania.
Afisa Uendelezaji Biashara SIDO Mkoa wa Shinyanga, Joseph Taban (wa pili kulia) akionesha sabuni za kuogea zilizotengenezwa na wajasiriamali kutoka kata za Ngokolo,Chamaguha, Ndala na Kambarage Manispaa ya Shinyanga waliopatiwa mafunzo ya vitendo yaliyotolewa na SIDO, NELICO na PACT Tanzania.
Meneja wa Vipindi na Mhariri Mkuu wa Kituo cha Matangazo Radio Faraja Fm Stereo, Simeo Makoba akizungumza wakati akifunga mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) kwa wajasiriamali kutoka kata za Ngokolo,Chamaguha, Ndala na Kambarage Manispaa ya Shinyanga yaliyoandaliwa na SIDO, NELICO na PACT Tanzania.

Wajasiriamali wakimsikiliza Meneja wa Vipindi na Mhariri Mkuu wa Kituo cha Matangazo Radio Faraja Fm Stereo, Simeo Makoba.
Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga, Hopeness Eliya  akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) kwa wajasiriamali kutoka kata za Ngokolo,Chamaguha, Ndala na Kambarage Manispaa ya Shinyanga yaliyoandaliwa na SIDO, NELICO na PACT Tanzania.

  Afisa Uchumi kutoka shirika la NELICO, Fortunatus Richard akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) kwa wajasiriamali kutoka kata za Ngokolo,Chamaguha, Ndala na Kambarage Manispaa ya Shinyanga yaliyoandaliwa na SIDO, NELICO na PACT Tanzania.

Afisa Uendelezaji Biashara SIDO Mkoa wa Shinyanga, Joseph Taban akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) kwa wajasiriamali kutoka kata za Ngokolo,Chamaguha, Ndala na Kambarage Manispaa ya Shinyanga yaliyoandaliwa na SIDO, NELICO na PACT Tanzania.
Ramadhan Hamis akisoma risala wakati wa kufunga mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) kwa wajasiriamali kutoka kata za Ngokolo,Chamaguha, Ndala na Kambarage Manispaa ya Shinyanga yaliyoandaliwa na SIDO, NELICO na PACT Tanzania.
Washiriki wa mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) wakiwa ukumbini.

Washiriki wa mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) kutoka kata ya Ngokolo wakipiga picha ya kumbukumbu na mgeni rasmi Meneja wa Vipindi na Mhariri Mkuu wa Kituo cha Matangazo Radio Faraja Fm Stereo, Simeo Makoba, viongozi wa SIDO na NELICO
Washiriki wa mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) kutoka kata ya Kambarage wakipiga picha ya kumbukumbu na mgeni rasmi Meneja wa Vipindi na Mhariri Mkuu wa Kituo cha Matangazo Radio Faraja Fm Stereo, Simeo Makoba, viongozi wa SIDO na NELICO
Washiriki wa mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) kutoka kata ya Chamaguha wakipiga picha ya kumbukumbu na mgeni rasmi Meneja wa Vipindi na Mhariri Mkuu wa Kituo cha Matangazo Radio Faraja Fm Stereo, Simeo Makoba, viongozi wa SIDO na NELICO
Washiriki wa mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) kutoka kata ya Ndala wakipiga picha ya kumbukumbu na mgeni rasmi Meneja wa Vipindi na Mhariri Mkuu wa Kituo cha Matangazo Radio Faraja Fm Stereo, Simeo Makoba, viongozi wa SIDO na NELICO.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments