VIONGOZI WA DINI MNAWAJIBU WA KUSIMAMIA MAADILI-WAZIRI SIMBACHAWENE

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu , Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene akizingumza wakati wa Uzinduzi wa Kambi ya Kanisa la Sabato Magomeni Mwembechai inayofanyika Kwembe Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Askofu wa Jimbo la Mashariki Kati Mwa Tanzania Joseph Mngwabi akitoa maelezo kuhusiana na kambi pamoja na shughuli za kambi wakati uzinduzi uliofanyika Kwembe Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Mchungaji wa Kanisa la Sabato Magomeni Mwembechai Methusela Masunga akizungumza kuhusiana na waliojipanga katika kwenda na kambi hiyo katika maombi na kuilishilisha neno la Mungu , jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu , Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene akipanda mti mara baada ya kuzindua Kambi ya Kanisa la Sabato Magomeni Mwembechai inayofanyika Kwembe Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu , Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene akipokea vitabu kutoka kwa viongozi wa Dini wa Kanisa la Sabato mara baada kuzindua Kambi ya Kanisa la Sabato Magomeni Mwembechai inayofanyika Kwembe Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Picha za pamoja za Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu , Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene pamoja makundi mbalimbali mara baada ya kuzindua Kambi ya Kanisa la Sabato Magomeni Mwembechai inayofanyika Kwembe Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.

Waumini wakimsikiliza Waziri Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu , Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene hayupo picha wakati wa uzinduzi wa Kambi ya Kanisa la Sabato Magomeni Mwembechai inayofanyika Kwembe Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.

*********************

*Viongozi wa dini wanena kwenda katika mafundisho zaidi kwenye masuala ya ndoa

Na Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera , Bunge na Uratibu George Simbachawene amesema kuwa kwa kipindi cha miezi tisa kwa eneo moja la Wilaya ya Temeke Ndoa 350 zimevunjika.

Simbachawene ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Kambi ya Kanisa la Sabato Magomeni linalofanyika Kwembe Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam.

Simbachawene amesema viongozi wa dini wana kazi ya kufanya kutokana na mmomonyoko wa maadili ambapo unachangia ndoa nyingi kuvunjika na kuwa na familia zinazolelewa na upande mmoja tu.

Amesema hali ndoa kuvunjika sio hali nzuri kwani takwimu hiyo ni Manispaa moja ya Temeke na hajajua hali ya nchi nzima ikoje ambapo viongozi wa dini wana kazi ya kufanya katika eneo la kujenga familia.

"Ndoa hizo zinafungwa na sherehe kubwa na kujipamba lakini hizo zinavunjika na viongozi wa dini wakiwa wanaziongoza kwa baraka naomba sasa viongozi wangu mkaliangalie hili katika kufundisha kwa ndo kuvunjika ni chukizo la Mungu"amesema Simbachawene.

Aidha amesema kuwa hata maendeleo yanafanywa na serikali haitakuwa ya maana kama familia zetu hazijengwa katika misingi ya uadilifu wa kuweza kusimamia maendeleo hayo.

Waziri Simbachawene amesema kuwa somo la ndoa liwe sehemu ya kambi hiyo kwani kuna vijana walioko katika ndoa na wengine wanatarajia kuingia na hao walio katika kambi wasiwe sehemu ya ndoa za kuvunjika. Hata hivyo Waziri Simbachawene ametaka waumini hao kushiriki Sensa kikamilifu .

Nae Askofu wa Jimbo la Mashariki Kati Mwa Tanzania Joseph Mngwabi amesema kuwa katika masuala yote katika kambo sehemu ya ndoa litakuwa la kipekee kwa kulifundisha kwa kufuata maandiko ya Mungu.

Amesema kuwa katika kipindi cha elimu juu ya sensa wamelipokea na watashiriki waumini wao katika kuendelea kuunga mkoa serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Hassan Suluhu.

Mchungaji wa Kanisa la Sabato Magomeni Mwembechai Methusela Masunga amesema kambi hiyo ni ya siku saba ambapo watafanya suala ibada pamoja ba kutoa huduma kwenye jamii.

Amesema Kanisa la Sabato Magomeni wako pamoja na Serikali kuendelea kuunga mkono kwa kila jitihada zinazofanyika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post