DC JOKATE ATOA PONGEZI KWA VIONGOZI WA KATA KUENDELEA KUHAMASISHA USHIRIKI WA ZOEZI LA SENSA

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe.Jokate Mwegelo akizungumza na baadhi ya viongozi wa wilaya hiyo pamoja na wawakilishi wa vyama vyote vya siasa kutoa kauli ya pamoja na muelekeo kuelekea siku ya sensa tarehe 23.08.2022. Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Ndg.Elihuruma Mabelya akizungumza na waandishi katika mkutano wa uliowakutanisha wadau mbalimbali, viongozi wa Wilaya ya Temeke wawakilishi wa vyama vyote vya siasa kutoa kauli ya pamoja na muelekeo kuelekea siku ya sensa tarehe 23.08.2022. Naibu Meya wa Temeke Bw.Arnold Peter akizungumza na waandishi katika mkutano wa uliowakutanisha wadau mbalimbali, viongozi wa Wilaya ya Temeke wawakilishi wa vyama vyote vya siasa kutoa kauli ya pamoja na muelekeo kuelekea siku ya sensa tarehe 23.08.2022. Viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Temeke pamoja na wawakilishi wa vyama vya siasa wakiwa katika mkutano na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe.Jokate Mwegelo kuzungumzia muelekeo wa siku ya Sensa ya Watu na Makazi ambayo inatarajia kufanyika tarehe 23.08.2022

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe.Jokate Mwegelo leo Agosti 19,2022 amekutana na baadhi ya viongozi wa wilaya hiyo pamoja na wawakilishi wa vyama vyote vya siasa kutoa kauli ya pamoja na muelekeo kuelekea siku ya sensa tarehe 23.08.2022.

Akizungumza katika kikao hicho, Mhe.Jokate amesema mitaa ambayo inaenda kuhesabiwa katika wilaya hiyo ni mitaa 142, hivyo amewataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa makarani wa sensa ili zoezi hilo liweze kwenda vizuri.

Aidha amewashukuru viongozi wa kata, viongozi wa dini pamoja na makundi mbalimbali kwenye wilaya hiyo ambao wamekuwa wakihamasisha na kusisitiza umuhimu wa kushiriki katika zoezi la sensa.

Pamoja na hayo Mhe.Jokate amesema wameandaa Tamasha kubwa ambalo litafanyika Agosti 20,2022 katika viwanja vya Zakhiem Mbagala lenye lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali ambao wataonesha vipaji na burudani mbalimbali zinazohamasisha sensa hivyo kupitia tamasha hilo anaimani wanatemeke wengi watahamasika na kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa.

Nae Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Ndg.Elihuruma Mabelya amewataka viongozi mbalimbali kwenye wilaya hiyo kuendelea kutoa ushirikiano katiika kuhamasisha jamii kushiriki katika zoezi la sensa ili idadi kamili iweze kupatikana kwaa maendeleo ya wanatemeke kwa ujumla.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post