TRC YAONGEZA SAFARI ZA TRENI KWENDA ARUSHA, KILIMANJARO NA TANGA


Neema kwa wasafiri wa Treni

SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limeongeza safari za Treni Kutoka Dar es salaam kwenda mikoa ya kaskazini ambayo ni Arusha, Kilimanjaro na Tanga kutoka safari mbili kwa wiki kama ilivyokuwa hapo awali mpaka safari tatu kwa wiki.


Kupitia taarifa yao TRC wamesema kwa sasa Treni itafanya safari zake siku za Jumatatu, Jumatano na Ijumaa saa nane na nusu mchana kutoka Dar es salaam kwenda Kaskazini, huku kutoka kaskazini kwenda Dar es salaam itafanya safari zake siku za Jumanne, Alhamisi na Jumamosi ikitoka Arusha saa nane na nusu mchana.

Usafiri wa Treni kwenda mikoani

Kuongezeka kwa safari hizo kumetokana na idadi ya watumiaji wa usafiri wa treni kuongezeka, hilo limekuja baada ya gharama za usafiri mwingine kupanda kutokana na ongezeko la bei ya mafuta ambapo inapelekea wananchi kutafuta gharama nafuu zaidi za usafiri.

Aidha, shirika limewaasa watumiaji wa usafiri huo kukata tiketi mapema ili kuepusha usumbufu.


Imeandikwa: John Mbwambo kwa msaada wa mitandao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post