Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima amekubali kuwa mlezi wa chama Cha Waandishi Wa Habari Mkoa Mwanza na kuahidi kushirikiana nao katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo.
Malima amekubali kuwa mlezi Klabu hiyo baada ya kuombwa na mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari kupokea kijiti hicho kutoka kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Robert Gabriel.
"Mimi nimevutiwa na utendaji wenu wa kazi na ndio maana mlivyoniita Leo nimekuja kuwasikiliza ila name Mimi nitawaita Ili niwaambie mambo yangu."alisema Malima
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mdahalo wa majadiliano juu ya umuhimu wa chanjo ya UVIKO 19 Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi Mkoa wa Mwanza Edwin Soko alimuomba Mkuu wa Mkoa kuwa mlezi wa Klabu hiyo ili pamoja na mambo mengine aweze kuwa mshauri Mkuu wa Klabu hiyo.
"Mhe. Mkuu wa Mkoa, huu umekuwa utamaduni wetu kila Mkuu wa Mkoa anayekuja Mwanza huwa tunamuomba kuwa mlezi wetu tukiamini kuwa ukaribu wetu unaweza kuwa na tija mwa Maendeleo ya Mkoa",amesema.