MREMBO AUAWA KWA KUCHOMWA MOTO AKILAZIMISHWA KUTOA MIMBA NA MUMEWE


Hana Mohamed Khodor; ni mrembo mwenye umri wa miaka 21 ambaye amekutana na umauti kwa kukataa kutoa mimba kwa shinikizo la mumewe.

Hana alikuwa mjamzito wa miezi mitano ambapo amefariki dunia baada ya kupokea kipigo kikali na kuchomwa moto na mumewe huyo, kisa kukataa kuitoa mimba husika.

Mume alitaka mimba itolewe kwa madai kwamba itaongeza mzigo wa gharama kwake kwani tayari walikuwa na watoto wawili.

Tukio hilo limejiri Kaskazini mwa Tripoli nchini Lebanon ambapo Hana amefariki dunia baada ya siku 11 za kupigania uhai wake akiwa hospitalini.

Habari kutoka nchini humo zinaeleza kuwa, baada ya kumpiga sana, mume alimchoma moto kupitia mtungi wa gesi na kumuunguza karibia asilimia 100% ya mwili wake ambapo madaktari walisema nafasi yake ya kupona ilikuwa finyu mno.

Akiwa hospitalini, ndugu wa mke ndiyo walikuwa wanahangaika huku na huko kupata pesa za gharama za matibabu ya operesheni na kuongezewa damu ili kunusuru maisha yake.
Shangazi wa Hana anasema kuwa, mume alimpiga mkewe kikatili mno.

Rafiki wa familia aliyefahamika kwa jina na Abdul Rahman amekiri tayari mume husika amedakwa na vyombo vya sheria baada ya kujaribu kukimbia nchini humo kufuatia ukatili alioufanya kwa Hana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post