KIMBUNGA CHAUA WATU 12Vimbunga vikali kabisa vimepiga katikati mwa bara la Ulaya na kupelekea vifo vya watu 12 wakiwemo watoto 3.

Vifo vingi vimesababishwa na miti iliyoanguka ambavyo vimeripotiwa katika nchi za Italia, Austria, pamoja na visiwa vya Ufaransa vya Corsica.

Mvua kubwa na upepo mkali vimepiga katika visiwa hivyo na kuleta uharibifu mbaya.

Majanga hayo ya kimbunga yanafuatia wiki kadhaa za ukame na joto kali lililorindima katika bara la ulaya.

Nyumba za watu zimeharibiwa vibaya, huku mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 13 akipoteza maisha kwa kuangulkiwa mna mti.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post