MARUBANI WAPITIWA USINGIZI ANGANI, NDEGE YAPITILIZA NJIA YA KUTUA


Marubani wawili walipitiwa na usingizi ndege ikiwa juu kwa umbali wa futi 37,000 (11,000m), na kupitiliza njia ya kutua ndege, chapisho moja la masuala ya anga limeripoti.

Muongoza ndege kwenye uwanja wa ndege wa Addis Ababa nchini Ethiopia walijaribu kuwasiliana na marubani hao bila mafanikio baada ya kona ndege ikipitiliza kwenye njia iliyopaswa kutua.

Hata hivyo marubani hao wa Shirika la Ndege la Ethiopia hatimaye waliamshwa na kengele maalumu (alarm) ya kujiendesha na kufanikiwa kutua kwenye njia ya pili katika uwanja huo huo, shirika la Aviation Herald lilisema.

Ndege ya abiria, Jumatatu iliondoka kutoka uwanja wa ndege wa Khartoum nchini Sudan. Ndege hiyo aina ya Boeing 737, yenye uwezo wa kubeba viti 154, kwa kawaida huchukua chini ya saa mbili katika safari yake kati ya nchi hizo jirani.

Muitikio wa watu kuhusu marubani hao kulala kazini zilichukulia kwa huruma na watu kutokana na ratiba ngumu ya kazi ya marubani.

"Siwezi kuwatupia lawama wafanyakazi wa Shirika la Ethiopia haswa hapa - hili ni jambo ambalo linaweza kumtokea mfanyakazi yoyote duniani na pengine ilitokea... Lawama ziko kwa shirika na wasimamizi," moja ya maoni yalisomeka kwenye Tovuti ya Aviation Herald.

"Uchovu wa marubani si jambo geni, na unaendelea kuwa tishio moja kubwa kwa usalama wa anga - kimataifa," alitweet mchambuzi wa masuala ya anga, Alex Macheras. BBC imewasiliana na Ethiopian Airlines kwa maoni.

Chanzo - BBC SWAHILI


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post