RAIS SAMIA ATEUA MAAFISA 22 KUWA MAJAJI WA MAHAKAMA KUU


NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameteua maafisa ishirini na wawili (22) kuwa Majaji wa Mahakama Kuu.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Bi. Zuhura Yunus kupitia taarifa aliyoitoa leo ameeleza kuwa,uteuzi huo umeanza Agosti 4,2022. Wafuatao ndiyo walioteuliwa;


Kevin David Mhina, kabla ya uteuzi huu Bwana Mhina alikuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani;


Gabriel Pascal Malata, kabla ya uteuzi huu Bwana Gabriel alikuwa Wakili Mkuu wa Serikali;


Adrian Philbert Kilimi, kabla ya uteuzi huu Bwana Adrian alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama;


Happiness Philemon Ndesamburo, kabla ya uteuzi huu Bi. Happiness alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama;


Victoria Mlonganile Nongwa, kabla ya uteuzi huu Bi. Victoria alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama;


Obadia Festo Bwegoge, kabla ya uteuzi huu Bwana Obadia alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama;


Ruth Betwel Massam, kabla ya uteuzi huu Bi. Ruth alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama;


Godfrey Ntemi Isaya, kabla ya uteuzi huu Bwana Godfrey alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama;


Gladys Nancy Barthy kabla ya uteuzi huu Bi. Gladys alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama;


Haji Suleiman Haji, kabla ya uteuzi huu Bwana Haji alikuwa Mwendesha Mashitaka Mfawidhi Mahakama Kuu, Zanzibar;


Fatma Rashid Khalfan, kabla ya uteuzi huu Bi. Fatma alikuwa Kamishna Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora;


Abubakar A. Mrisha, kabla ya uteuzi huu Bwana Abubakar alikuwa Wakili wa Serikali;


Lusungu Hemed Hongoli, kabla ya uteuzi huu Lusungu alikuwa Wakili Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali;


Monica Peter Otaru, kabla ya uteuzi huu Bi. Monica alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali;


Kamana Stanley Kamana, kabla ya uteuzi huu Bwana Kamana alikuwa Mkurugenzi Msaidizi (TAMISEMI);


Hamidu Rajabu Mwanga, kabla ya uteuzi huu Bwana Hamidu alikuwa Mkurugenzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi;


Marlin Leonce Komba, kabla ya uteuzi huu Bi. Marlin alikuwa Mkurugenzi wa Sheria, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi;


Dkt. Mwajuma Kadilu Juma, kabla ya uteuzi huu Dkt. Mwajuma alikuwa Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu Mzumbe;


Dkt. Cleophas K.K. Morris, kabla ya uteuzi huu Dkt. Cleophace alikuwa Mhadhiri, Chuo Kikuu Dar es Salaam;


Asina A. Omari, kabla ya uteuzi huu Bi. Asina alikuwa Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na ni Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC);


Aisha Zumo Bade, kabla ya uteuzi huu Bi. Aisha alikuwa Wakili wa Kujitegemea; na
Mussa Kassim Pomo, kabla ya uteuzi huu Bwana Mussa alikuwa Wakili wa Kujitegemea.


Tarehe ya uapisho wa Majaji Wateule itatangazwa baadaye.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post