WAZIRI MKUU MSTAAFU AFARIKI GEREZANI


Lounceny Camara

WAZIRI wa zamani wa Guinea Lounceny Camara alikuwa tayari amelazwa hospitali mara moja kabla ya kufungwa jela mwezi Mei, chanzo cha kifo chake kilitokana na kupatwa na kiharusi Ijumaa na alifariki hospitalini jioni iliyofuata, kaka yake alithibitisha.


Familia ya Lounceny Camara ilikata rufaa mahakamani bila mafanikio ili Camara aruhusiwe kusafiri nje ya nchi kupata matibabu, ameongeza kaka yake alie kuwa anatoa taarifa.

Kanali Mamady Doumbouya, Rais wa Guinea

Lounceny Camara,aliekuwa na umri wa miaka 62, ni kati ya mawaziri wa zamani na maafisa waandamamizi walioshtumiwa ubadhilifu wa pesa za umma na kufungwa jela baada ya jeshi kumuondoa madarakani Rais wa zamani Alpha Conde mwaka uliopita.Imeandikwa:Leokadia Charles kwa msaada wa mtandao

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post