AMUUA MKEWE KWA KUMPIGA NA KUMNG'ATA KIDEVU UKWENI KWENYE MSIBA


Sehemu ya mauaji yalipofanyika
**

Mariam Masanja 22, mkazi wa Kijiji cha Nyabugela, Kata ya Mganza wilayani Chato mkoani Geita, ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na kung'atwa kidevu na mme wake Edward Franscis 20, ambao walikutana kwenye familia ya mwanamke kuhani msiba baada ya ugomvi wao wa muda mrefu.

Wawili hao walikutana kwenye msiba wa kaka wa marehemu ambapo marehemu alikuwa mkoani Mwanza kwa dada yake baada ya kugombana na mme wake ndipo aliporudi kwao baada ya kusikia kaka yake amefariki.

Wazazi wa marehemu wameeleza walivyopata taarifa za mtoto wao kuuawa na mme wake huku baba mzazi wa marehemu anasema wawili hao walikuwa na ugomvi wa mara kwa mara wa wivu wa kimapenzi.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyabugela Metusela Mgema, amesema wawili hao walifika mara kadhaa kwenye ofisi yake kwa ajili ya migogoro ndani ya familia yao ambayo ilikuwa inasuruhishwa mara kwa mara lakini mpaka kufikia kifo cha mwanamke wawili hao walikuwa wameachana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

1/Post a Comment/Comments

Post a Comment