RAIS AWASIMAMISHA KAZI MAWAZIRI WATATU KWA UFISADI


Mawaziri waliosimamishwa kazi
Rais wa Liberia George Weah

RAIS wa Liberia na mchezaji wa zamani wa soka George Weah amewasimamisha kazi maafisa watatu kwa kosa la ufisadi.


Hiyo ni baada ya serikali ya Marekani kutangaza kuwawekea vikwazo kwa tuhuma za rushwa na ufisadi wa mali za umma.

Maafisa hao ni Nathaniel McGill aliyekuwa Waziri wa nchi na Mkuu wa wafanyakazi wa Rais anaedaiwa kutishia wapinzani na utumiaji mbaya wa mali ya Umma, Bill Twehway ambae ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kitaifa ya Bandari yeye anadaiwa kwa kuingiza pesa za Bandari katika akaunti yake binafsi, na afisa wa tatu ni Jenerali Seyma Serenius Cyphus.


“Rais Weah anaona tuhuma dhidi ya maafisa waliomo kwenye ripoti hiyo kuwa nzito. Kutokana na hali hiyo, Rais George Manneh Weah amewasimamisha kazi maafisa hao Waziri wa Nchi Nathaniel McGill, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari ya Kitaifa Bill Twehway na Wakili Jenerali Seyma Serenius Cyphus na athari ya haraka ili kuwawezesha kukabiliana na uchunguzi.”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post