POLISI WAUPATA MWILI WA JAMAA ALIYEZAMA MTONI AKIOKOA MTOTO

Polisi nchini Uganda wameupata mwili wa raia wa Uingereza alifariki kwa kuzama kwenye mto Nile siku ya Jumatano.


Robert Kaweesi, 48, kutoka Birmingham, alikuwa na mkewe, Justine Katantazi, na watoto wao wanne na walifikia kwenye moja ya hoteli iliyoko kando ya kingo za mto huko Pakwach. 

Mwanawe mwenye umri wa miaka 12 alienda kuogelea mtoni lakini alipopatwa na matatizo, babaake aliruka ili kumsaidia.

Hata hivyo Mvulana huyo aliokolewa na watu waliokuwa karibu lakini Bw Kaweesi hakuweza kuonekana, polisi walisema awali.

Mwili wake ulipatikana Ijumaa asubuhi kufuatia msako wa wapiga mbizi wa polisi na watu wa kujitolea wa eneo hilo. 

Bw Kaweesi, raia wa Uingereza mwenye asili ya Uganda, na mpenzi wake wa muda mrefu Justine Katantazi walifunga ndoa nchini Uganda mapema Agosti. 

Bi Katantazi alimtaja Kaweesa kama mtu mcheshi na rafiki yake mkubwa.

Wizara ya mambo ya nje ya Uingereza ilisema inaisaidia familia hiyo na ilikuwa inawasiliana na mamlaka za ndani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post