RAIS SAMIA : MWANANGU CHALAMILA MATEGEMEO YANGU UMEKUA SASA, AKILI IMETULIA

 

Rais Samia Suluhu Hassan na Albert Chalamila (kulia).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Albert John Chalamila kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Agosti, 2022.

Na Kadama Malunde  - Malunde 1 blog

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert Chalamila  atulize akili na kwenda kumsaidia kufanya kazi katika eneo alilompangia.


Rais Samia amesema hayo leo Jumatatu Agosti 1,2022 wakati akiwaapisha wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa aliowateua hivi karibuni.

"Mwanangu Chalamila mategemeo yangu umekua sasa, akili imetulia wewe ni mfanyakazi mzuri lakini mtundu mno, sasa nilikuacha nje kidogo kipindi hicho nimeamua kukurudisha naomba ukakue,ukue akili itulie uende ukafanye kazi ukanisaidie eneo ulilopangiwa na hii haina maana kwamba umemaliza ukikaa umekaa, nakuangalia kwa ukaribu sana",amesema Rais Samia.


Hivi karibuni Rais Samia alimteua Albert Chalamila kuwa mkuu wa mkoa wa Kagera baada ya kutengua uteuzi wake akiwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza Juni 11,2021.


"Ninapofanya teuzi hizi siangalii mambo mengine, Siangalii kabila, rangi ya mtu, anakotoka ninachoangalia ni sifa, uwezo, uaminifu wake kwa nchi na Serikali", amesema Rais Samia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post