WAUAWA KWA KUCHOMWA MOTO TUHUMA ZA KUIBA NG'OMBE SHINYANGA


Watu wawili wameuawa kwa kupigwa na kisha miili yao kuchomwa moto na watu wenye hasira kali , baada ya kutuhimiwa kwa wizi wa Ng’ombe katika kijiji cha Mwamala (B) kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Mtendaji wa Kata ya Mwamala Suzana Kanyange ameiambia Redio Faraja kuwa, tukio hilo limetokea majira ya saa 12:30 asubuhi ya leo, ambapo watu hao walizingirwa na wananchi baada ya kutuhumiwa kuwa wamekuwa wakijihusisha na matukio ya wizi wa Ng’ombe kijijini hapo.

Amewataja waliouawa kuwa ni, Simbili Philipo Izengo mwenye umri wa miaka 33 na Kashinje Malulu mwenye umri wa miaka 32, ambao wote ni wakazi wa kijiji cha Mwamala (B) katika halmashauri hiyo ya wilaya ya Shinyanga.

CHANZO - RADIO FARAJA BLOG

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post