KAULI YA KWANZA YA MKE WA MAREHEMU AUGUSTINO MREMA


Kufuatia kifo cha aliyekuwa mwanasiasa mkongwe na mwenye wa chama cha TLP Augustino Lyatonga Mrema, mke wake Doreen amefunguka haya.


“Namshukuru Mungu kwa maisha aliyompatia hapa duniani na kipindi ambacho nilipata nafasi ya kuwa naye pamoja.
Nitakumbuka vitu vingi kutoka kwake, siwezi kuvisema kwa sasa, ila yule ni mume wangu, rafiki yangu, mpenzi wangu, alikuwa mshauri na mwalimu wangu, ni vingi ambavyo namkumbuka navyo kwa sasa siko sawa kuongea ila nikikaa vizuri nitaongea na Watanzania,” alisema Doreen.


“Kwa sasa ninachoweza kusema ni kuwashukuru watu wote waliokuwa wakimuombea mume wangu wakati wa ugonjwa, lakini pia niwashukuru wote ambao mnaendelea kuungana nasi katika kipindi hiki kigumu sana kwetu, naomba tuendelee kumuombea apumzike kwa amani,” alisema


Mrema alifariki dunia Jumapili Agosti 21, 2022, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu, ameacha mke na watoto watano.


Mwili wa marehemu Agustino Mrema unatarajiwa kuzikwa kesho Alhamis mkoani Kilimanjaro

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post