Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima amewataka wanahabari wa Mkoa wa Mwanza kuwa kioo chake katika kipindi chote Cha uongozi wake.
Ameyasema hayo wakati akifungua rasmi mdahalo wa majadiliano juu ya umuhimu wa chanjo ya UVIKO 19 ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi Wa Habari Mkoa wa Mwanza na Internews Tanzania.
Malima amewahakikishia wanahabari ushirikiano huku akiwataka kuandika habari zitakazochochea Maendeleo ya Mkoa wa Mwanza kwa ujumla.
"Mkiandika habari za kuchochea Maendeleo mtakuwa rafiki zangu lakini mkiandika habari mbaya tu kila kiku sitafanya kazi na nyie nitawatafuta wale tunaoendana."alisema Malima.
Akizungumzia zoezi linaloendelea la uchanjaji wa chanjo ya UVIKO 19 Malima amewataka wanahabari kuhakikisha wanaandika zitakazo washawishi wananchi kujitokeza kuchanja.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mwanza Press Club Edwin Soko ameahidi kuendelea kushirikiana na serikali ya Mkoa wa Mwanza katika kampeni mbalimbali ikiwemo ya chanjo ya UVIKO 19.
"Tulishiriki vema katika uzinduzi wa chanjo ya UVIKO 19 na baadhi ya Waandishi walichanja na tukaendelea kuripoti namna zoezi la chanjo linavyoendelea,huu ni utamaduni wetu tutahakikisha elimu inawafikia wananchi.alisema Soko.
Kwa upande wao washiriki wa mdahalo huo wameiomba Klabu ya Waandishi Wa Habari Mkoa Mwanza pamoja na Internews kuwapatia mafunzo ya mara kwa mara kwa kuwa Mkoa wa Mwanza una waandishi wengi ambao wote wanahitajika kupewa elimu.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza, Edwin Soko