WAZIRI MKENDA AUTAKA UONGOZI WILAYANI RUNGWE KUTENGA ENEO MAPEMA KWA AJILI YA UJENZI WA VETA

 



Na Mathias Canal, Kiwira-Mbeya

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof Adolf Mkenda ameutaka uongozi wa Wilaya ya Rungwe kutafuta eneo la zaidi ya Hekari 20 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa chuo cha ufundi stadi-VETA.

Waziri Mkenda ameyasema hayo leo tarehe 7 Agosti 2022 alipopewa fursa ya kujibu hoja zilizoibuka wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan Wilayani Rungwe ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani Mbeya iliyoanza tarehe 5 Agosti  2022 hadi tarehe 8 Agosti 2022.

Waziri Mkenda amesema kuwa Katika bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mwaka 2022/2023 zimetengwa Bilioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa Vyuo vya Ufundi stadi-VETA katika wilaya mbalimbali nchini hivyo Wilaya ya Rungwe ni mojawapo katika mpango huo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments