SATURA : TUNAENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA KIJAMII MANISPAA YA SHINYANGA ILI KULINDA HADHI YA MAKAO MAKUU YA MKOA


Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Jomaary Satura akizungumza kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kilichofanyika leo Jumatatu Agosti 22,2022.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Jomaary Satura amesema Maboresho ya huduma za kijamii yanayoendelea katika Manispaa ya Shinyanga ni sehemu ya mikakati ya kuendelea kulinda hadhi ya Makao Makuu ya Mkoa wa Shinyanga.

Satura amesema hayo leo Jumatatu Agosti 22,2022 wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

“Jukumu la msingi tulilo nalo ni kuwaletea wananchi maendeleo, kubwa zaidi ni uboreshaji wa huduma za kijamii na mahitaji mengine ya kijamii sambamba na kukuza uchumi na katika hili la kukuza uchumi kuna kilimo, mifugo na biashara”,amesema Satura.

“Fursa kuu tuliyonayo sisi Manispaa ya Shinyanga ni kuwa makao Makuu ya Mkoa wa Shinyanga. Sisi hatuna madini lakini pia changamoto ya Kijiographia, hali hii imesababisha tuwe na mzunguko duni wa kibiashara. Tunaendelea kuboresha muonekano wa mji wetu kwani hii ndiyo fursa iliyopo kwenye Manispaa ya Shinyanga ili kuendelea kulinda hadhi ya Makao Makuu ya Mkoa”, ameeleza.

Ameongeza kuwa Maboresho ya huduma za kijamii yanayoendelea katika Manispaa ya Shinyanga ni endelevu ili kusitiri manispaa ya Shinyanga.

“Tuna haja ya kuifanya Manispaa yetu ili iendelee kuwa na hadhi ya Makao Makuu ya Mkoa wa Shinyanga. Jitihada tunazoendelea nazo katika kuboresha huduma za kijamii ni kubakiza hadhi ya Makao Makuu ya Mkoa na tuna nafasi ya kuwa Soko ili kuwa na fursa ya kibiashara”,amesema.

“Tuna mpango wa kuanzisha taasisi za elimu ya Juu… Chuo chetu cha Ushirika Tawi la Kizumbi Shinyanga kimetengewa  Shilingi Bilioni 11  ambazo zitaletwa na Serikali kuboresha miundo mbinu ili chuo kiwe na hadhi ya Chuo Kikuu. Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto pia nacho tunaangalia namna ya kukipandisha hadhi kiwe Chuo Kikuu”,ameongeza Satura.


Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko amesema maendeleo katika Manispaa ya Shinyanga yanakua kwa kasi hivyo wataendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuongeza nguvu na mshikamano zaidi kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akizungumza wakati akifungua Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kilichofanyika leo Jumatatu Agosti 22,2022. Kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Jomaary Satura, kulia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Esther Makune. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akizungumza wakati akifungua Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kilichofanyika leo Jumatatu Agosti 22,2022.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akizungumza wakati akifungua Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kilichofanyika leo Jumatatu Agosti 22,2022.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Jomaary Satura akizungumza kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kilichofanyika leo Jumatatu Agosti 22,2022.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Jomaary Satura akizungumza kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kilichofanyika leo Jumatatu Agosti 22,2022. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akifuatiwa na Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Esther Makune na Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Jomaary Satura.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi akizungumza kwenye kikao cha baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi akizungumza kwenye kikao cha baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi (katikati) na Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Esther Makune (kushoto) wakiandika dondoo muhimu wakati wa kikao cha baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Jomaary Satura (kulia), Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akifuatiwa na Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Esther Makune na Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Jomaary Satura wakiwa kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga.
Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kikiendelea
Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kikiendelea
Watumishi wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Watumishi wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kikiendelea.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Grace Ntungi akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga


Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post