WAANDISHI WA HABARI WAKUMBUSHWA KUHAMASISHA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA COVID - 19


Mjumbe wa Kamati Tendaji Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena, akitoa mafunzo kwa Wanahabari Juu ya habari za UVIKO-19.
Mjumbe wa Kamati Tendaji Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena, akitoa mafunzo kwa Wanahabari Juu ya habari za UVIKO-19.

Na Marco Maduhu, DODOMA

Wanahabari kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini, wamepewa mafunzo ya kuandika habari za kuhamasisha wananchi kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona( UVIKO-19) pamoja na kupata chanjo.

Mafunzo hayo yametolewa leo Agosti 18, 2022 Jijini Dodoma na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), kwa kushirikiana na Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF).

Mwezeshaji wa mafunzo hayo Juliana Mshama kutoka Kitengo cha Elimu kwa Umma kutoka Wizara ya Afya, akielezea Mwenendo wa UVIKO-19 hapa nchini, amesema wanahabari hapa nchini wanapaswa kuendelea kuhamasisha wananchi kujikinga na ugonjwa huo pamoja na kupata chanjo.

“Tanzania bado tuna visa vya watu kupata maambukizi ya ugonjwa wa UVIKO-19, hivyo jamii bado inapaswa kuendelea kuelimishwa juu ya kuchukua tahadhari ya kujikinga lakini pia kupata chanjo,”amesema Mshama.

Aidha, amesema lengo Tanzania hadi kufikia Disemba 2022, Serikali inatarajia kuchanja watu milioni 21 sawa na asilimia 70 ya Watanzania wenye umri wa miaka 18.

Amesema pamoja na juhudi zinazofanywa za kuwafikia wananchi ilikupata chanjo kamili, bado kuna changamoto ya watu kurudi kupata dozi ya pili, ambapo takwimu zinaonesha watu 449,416 sawa na asilimia 26 ya watu Milioni 1.7 waliotakiwa kurudi kwa ajili ya dozi ya pili ya PFIZER, hawakurudi kwa kipindi cha Julai 31 mwaka huu.

Kwa upande wa chanjo ya Sinopharm watu 325,982 sawa na asilimia 13, kati ya watu 2,439,250 hawakurudi kwa ajili ya kupata dozi ya pili.

Naye Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena amewataka wanahabari wanapokuwa wanaandika taarifa zao, wajikite kuandika habari kwa undani zaidi na kuzielezea kwa kina na siyo kuishia kuandika taarifa nyepesi.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo Juliana Mshama kutoka Kitengo cha Elimu kwa Umma kutoka Wizara ya Afya, akitoa mafunzo kwa Wanahabari.
Mwezeshaji Catherine Itige kutoka Wizara ya Afya akitoa mafunzo kwa Wanahabari.
Wanahabari wakiwa kwenye mafunzo.
Wanahabari wakiwa kwenye mafunzo.
Wanahabari wakiwa kwenye mafunzo.
Wanahabari wakiwa kwenye mafunzo.
Wanahabari wakiwa kwenye mafunzo.
Wanahabari wakiwa kwenye mafunzo.
Wanahabari wakiwa kwenye mafunzo.
Wanahabari wakiwa kwenye mafunzo.
Wanahabari wakiwa kwenye mafunzo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post