WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAJIPANGA KUSHIRIKIANA NA WADAU WA SEKTA YA UTALII


Waziri wa maliasili na utalii Balozi Dkt. Pindi Chana akiongea katika mkutano wa wadau wa sekta ya utalii (MPPD)leo mkoani Arusha.

Na Woinde Shizza , ARUSHA

SERIKALI kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imejipanga
kushirikiana na wadau wa sekta binafsi kujadili mapendekezo ya sera sheria taratibu na kanuni kwa lengo la kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini ikiwemo biashara ya Utalii ambapo imedhamiria kuboresha mazingira ya biashara hiyo.


Aidha Serikali imejipanga kuhakikisha inatengeneza mfumo wa pamoja wa biashara baina ya wadau wa Utalii ikiwa ni lengo la kupata huduma zote sehemu moja za tozo kodi na malipo yote ya sekta hiy o(One stop Shop) ili sekta hiyo ichangie kikamilifu katika uchumi.


Akiongea wakati akifungua mkutano wa Wadau wa sekta ya Utalii (MPPD) Jijini Arusha Waziri wa Maliasili na Utalii balozi Dkt, Pindi Chana amesema kwamba maagizo aliyotoa Mh.Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa 13 wa baraza la taifa la biashara TNBC jijini Dodoma alituagiza tukutane na sekta binafsi hususani sekta ya Utalii kujadili mapendekezo na mageuzi ya sera sheria kwa lengo la kuboresha mazingira ya biashara hiyo.


Amesema kwamba serikali imedhamiria kwa dhati kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji katika sekta ya Utalii ili ichangie kikamilifu katika uchumi na maendeleo ya Taifa letu kwa ujumla pia dhamira hii inaenda sambamba na uendelezaji wa malengo a kimkakati ya mpango wa Tanzania The Royal Tour katika kukuza Utalii kadhalika na Uhifadhi wa maliasili na malikale zetu.


Awali akiongea wakati akimkaribisha Waziri Chana katika kikao hicho Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof.Eliaman Sedoyeka alisema kwamba kupitia wizara hiyo wamejipanga kuongeza juhudi kubwa za kuutangaza Utalii duniani ikiwa ni ishara ya kuunga juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan aliyefanya kwa vitendo kuandaa Filamu ya The Royal
Tour.
Amesema pamoja na sekta hiyo kuathiriwa na uwepo wa janga la Uviko 19 sanjari na vita baina ya mataifa ya Urusi na Ukrein bado wizara itaendelea kupanua soko la utalii kufikia malengo ya watalii milion 5 mwaka 2025.


Kwa Upande wake Mshauri wa Mazingira ya Uwekezaji IFC Anita Kundy amesema kwamba Tangu 1956, IFC imewekeza zaidi ya dola bilioni 2.8 katika miradi zaidi ya 260 katika nchi 89 na zaidi ya nusu ya uwekezaji huu katika nchi nyingine. Nchini Tanzania, tumewekeza pia katika hoteli jijini Dar es Salaam.


Kwa mujibu wa Dunia na Baraza la Utalii, kila dola inayotumika kwa usafiri na utalii inazalisha zaidi ya dola tatu za pato la kiuchumi.

Zaidi ya wafanyakazi milioni 100 wameajiriwa katika sekta hii duniani kote, na mapato ya utalii yanachangia mtiririko wa fedha zaidi kwa nchi zinazoendelea kuliko mtiririko wote wa misaada kutoka kwa wafadhili wa kigeni.


Alisema IFC inafuraha kuunga mkono na kusapoti kufikiwa kwa malengo muhimu ya serikali ya awamu ya 6 ya kuifanya Tanzania kama kivutio cha utalii na uwekezaji. Kwa miaka sitini, IFC, mwanachama wa Benki ya Dunia, imefanyakazi na sekta binafsi kwenye kuleta masuluhisho yaliyoleta mabadiliko chanya kijamii na kiuchumi.
Kwa Mujibu wa Kundy amesema imefanikisha hili kwa kuunda masoko mapya,kuhamasisha wawekezaji binafsi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post