MKUTANO WA DHARURA WA BARAZA LA MAWAZIRI WA NCHI ZINAZOZALISHA ALMASI (ADPA)KUFANYIKA KESHO JIJINI ARUSHA

 
Dkt. Doto Biteko

Na Woinde Shizza , ARUSHA 

Tanzania Kama mwenyekiti na mwenyeji wa mkutano wa tatu wa dharura wa baraza la mawaziri wa nchi zinazozalisha Almasi (ADPA) kesho Julai 29  itafanya mkutano wa baraza la mawaziri katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Arusha (AICC).


Hayo yameelezwa jijini Arusha leo na waziri wa madini, Dkt. Doto Biteko wakati akiongea na vyombo vya habari kuhusu mkutano wa tatu wa dharura wa baraza la mawaziri wa jumuiya ya nchi za Afrika zinazozalisha madini ya Almasi.


Waziri Dkt. Biteko alisema kikao hicho kitatanguliwa na kikao cha kamati ya wataalamu ambacho kimekaa leo kupitia taarifa na nyaraka na kabla ya kuwasilisha kwenye baraza.

"Lengo la mkutano huu pamoja na mambo mengine ni kuidhinisha nyaraka muhimu za ADPA zilizofanyiwa marekebisho ambazo ni katiba, kanuni na miongozo ya umoja huo na kuteua viongozi watatu wa Sekretarieti ambao ni katibu Mtendaji na manaibu wake wawili", amesema Dkt. Biteko.

Dkt Biteko alisema jumuiya ya wazalishaji wa Almasi Afrika (ADPA) ilianzishwa kwa mujibu wa azimio la Luanda, Angola mnano November 2006 na lengo kuu la kuundwa kwa ADPA ni kuzipatia nchi zinazozalisha Almasi Afrika jukwaa la kuzikutanisha nchi zote za Afrika katika kusudi moja la kuhakikisha rasilimali za madini hayo zinanufaisha nchi wanachama pia zinapokutana nchi wanachama zinazhirikiana uzoefu na ushirikiano katika nyanja anuwai za Sekta ya almasi.

Aidha Dkt. Biteko alibainisha kuwa katika kipindi hicho chote Tanzania ni mwenyeji wa jumuiya hiyo imekuwa ni heshima kubwa kwa kuwajibika kwa ajili ya marndeleo ya nchi, hususani katika usimamizi wa madini ya almasi ambapo kama ilivyoahidi nchi ya Tanzania wakati ikikabidhiwa nafasi hiyo imewezesha kupitiwa kwa mfumo wa jumuiya hiyo ikiwepo marekebisho ya katiba na kanuni pia miongozo mbalimbali ya jumuiya.

Dkt Biteko amebainisha kuwa kama nchi imejifunza zaidi kuhusu usimamizi wa sekta hususani kwa madini ya Almasi ambapo pia nchi wanachama na hata wasio wanachama walipata nafasi ya kuja kujifunza kuhusu namna Tanzania ilivyofanikiwa kuwaendeleza wachimbaji wadogo wakiwepo wa madini ya almasi na madini ya dhahabu na namna ambavyo Serikali ilivyoweza kusimamia mifumo inayohusisha mnyororo mzima wa shughuli za madini.

Alisema nchi ya Tanzania inatarajia kukabidhi uenyekiti wa jumuiya ya wazalishaji wa almasi(ADPA) kwa nchi ya Zimbabwe kwa kuwa Tanzania ilichaguliwa kuwa mwenyekiti wa Baraza la mawaziri wa ADPA toka mwaka 2021.

Uenyekiti huo utakabidhiwa Machi 2023,ambapo makabidhiano rasmi ya uenyekiti yatafanyika rasmi katika mkutano wa nane wa kawaida wa baraza la mawaziri wa nchi zinazozalisha almasi Afrika(ADPA) utakaofanyika katika jiji la Victoria falls nchini Zimbabwe.


Biteko alieleza kuwa katika kipindi ambacho Tanzania imekuwa  mwenyekiti wa jumuiya hadi sasa  imeweza kupata heshima kubwa ya  kuwajibika kwa ajili maendeleo hususani katika usimamizi wa madini ya Almasi.

Alisema kuwa wameweza kupitia  upya kwa mifumo ya jumuiya hiyo ikiwemo marekebisho ya katiba,kanuni na miongozo mbalimbali ya jumuiya.

"Tulikabidhiwa uenyekiti na tunaweza kusema kuwa tumefanya makubwa sana ila tutashuhudia uteuzii wa viongozi watatu wa taasisi watakao isimamia kwa mujibu wa katiba"alisema.

Waziri Biteko aliongeza kuwa kama nchi wameweza kujifunza zaidi usimamizi wa sekta hususani kwa madini ya almasi ambapo pia nchi wanachama na hata wasio wanachama walipata nafasi ya kuja kujifunza Tanzania namna ilivyofanikiwa kuwaendeleza wachinbaji wadogo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post