NaCoNGO, WORKING GROUP ZAKUTANISHA NGO's ZA SHINYANGA KUJADILI NAMNA YA KUJIKWAMUA KIUCHUMI


Mbunge wa Jimbo la Kahama Jumanne Kishimba akizunguza kwenye Warsha ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali mkoani Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Baraza la NGO Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na Mashirika yanayofanya kazi za kupinga ukatili wa kijinsia Mkoani Shinyanga (TAPO), yameendesha warsha ya siku moja kujadili namna ya kujikwamua kiuchumi na kufanya shughuli zao za kijamii bila ya kutegemea fedha za wafadhili pekee.

Warsha hiyo imefanyika leo Julai 24, 2022 katika ukumbi wa mikutano Karena Hotel, huku Mgeni Rasmi akiwa ni Mbunge wa Jimbo la Kahama Jumanne Kishimba.

Akizungumza kwenye Warsha hiyo Mjumbe wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali (NaCoNGO) mkoani Shinyanga Mussa Ngangala, amesema wamefanya mkutano huo ili kujadili mifumo endelevu ya kifedha kwenye taasisi na kuinuka kiuchumi pamoja na kufanya kazi kulingana na mazingira halisi.

Ngangala ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la (TVMC), amesema Mashirika ya yasiyo ya kiserikali hayatengenezi faida kwenye shughuli zao (Non profit), na ndiyo maana mengi hujiendesha kuendesha kwa kutegemea fedha za wafadhili, na wakiondoka wafadhili hao huyumba na kushindwa kufanya kazi.

“Mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Shinyanga yamekutana hapa leo kufanya warsha ya siku moja, ili kujadiliana masuala ya kiuchumi na jinsi ya utendaji wetu kazi kulingana na mazingira halisi, na kuboresha shughuli zetu za kuhudumia jamii,”amesema Ngangala.

Naye Mwenyekiti wa TAPO mkoani Shinyanga Jonathan Manyama, amesema imefikia wakati sasa mashirika yasiyo ya Kiserikali kufikiria nje ya boksi, na kuanzisha vyanzo vingine vya mapato na siyo kuendesha shughuli zao kwa kutegemea fedha za wahisani pekee, ili siku fedha hizo zisipopatikana wasiweze kuyumba na kushindwa kutoa huduma kwa jamii.

“Tunaiomba Serikali iangalie pia namna ya kuziwesha Ruzuku Asasi za kiraia kama wanavyofanya nchi ya Rwanda, sababu shughuli hizi zinazofanywa siyo kazi za mashirika bali ni kazi ya Serikali,”amesema Manyama.

Aidha, Mratibu wa Mfuko wa Ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT-Trust) Glory Mbia, naye amekazia suala hilo la Asasi za kiraia kupewa Ruzuku na Serikali, na kutolea mfano kama ilivyofanywa na Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) ambapo iliyawezesha mashirika fedha kwa ajili ya kutoa elimu ya uchaguzi kwa wananchi.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi kwenye Warsha hiyo Mbunge wa Jimbo la Kahama Jumanne Kishimba, ameyapongeza mashirika yasiyo ya kiserikali kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya ndani ya jamii.

Akizungumzia suala la uchumi, amewasihi wawekeze kwenye miradi ya ufugaji ng’ombe, miti ya kuni na mkaa, miradi ambayo itawainua kiuchumi, na kuacha kufanya shughuli zao kwa kutegemea fedha za wahisani pekee.

Aidha, katika Warsha hiyo zimetolewa nasaha mbalimbali katika utendaji kazi wa Asasi za kiraia, likiwamo suala la uwazi katika matumizi ya fedha, uvumilivu, ubunifu, kujitoa, uaminifu, kujitambua, pamoja na kushikamana.

Mbunge wa Jimbo la Kahama Jumanne Kishimba akizunguza kwenye Warsha ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali mkoani Shinyanga.

Mjumbe wa Baraza la Taifa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NACONGO) kutoka mkoani Shinyanga Mussa Ngangala akizungumza kwenye Warsha hiyo.

Mwenyekiti wa muunganiko wa mashirika yasiyo ya Kiserikali mkoani Shinyanga (TAPO) Jonathan Manyama akizungumza kwenye Warsha hiyo.

Meza kuu wakiwa kwenye Warsha hiyo.

Wachokoza mada kwenye Warsha hiyo.

Mbunge wa Jimbo la Kahama Jummane Kishimba, (kushoto) akiwa na Mjumbe wa NACONGO Mussa Ngangala kwenye Warsha hiyo.

Warsha ikiendelea.

Warsha ikiendelea.

Warsha ikiendelea.

Warsha ikiendelea.

Warsha ikiendelea.

Warsha ikiendelea.

Warsha ikiendelea.
Warsha ikiendelea.

Warsha ikiendelea.

Washiriki wakiwa kwenye Warsha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments