Tanzia: MSANII WA FILAMU BI. SONIA AFARIKI DUNIA



Msanii wa filamu nchini Tanzania Farida Sabu maarufu kwa jina la 'Bi Sonia' amefariki dunia.

Bi Sonia ambaye alijulikana sana kupitia kikundi cha Kaole Sanaa group amefariki leo, mjini Zanzibar ambapo alikuwa anauguzwa na mwanae.

Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji, Chiki Mchoma amethibitisha taarifa hizo, huku msiba ukitarajiwa kufanyika huko huko Zanzibar.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post