TEITI YATOA ELIMU KWA WANANCHI NAMNA INAVYOTIMIZA MAJUKUMU YAKE KWA MUJIBU WA SHERIA


Kamishna Msaidizi Tume ya Madini Tanzania na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la vyama vya wachimbaji wadogo wa madini (FEMATA) Haroun Kinega (kulia) akimsikiliza Afisa Msimamizi wa Fedha wa Taasisi ya Uhamasishaji, Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali madini, Mafuta na Gesi asilia (TEITI) Erick Ketagory (kushoto) alipokuwa katika Banda lao lililopo ndani ya banda kuu la STAMICO katika maonesho ya sabasaba leo Julai 11,2022 Jijini Dar es salaam.

Kamishna Msaidizi Tume ya Madini Tanzania na Afisa Mtendaji Mkuu wa (FEMATA) Haroun Kinega (kulia) akitia saini kwenye kitabu cha wageni mara baada ya kumaliza ziara yake fupi katika Banda hilo.

Afisa Msimamizi wa Fedha wa Taasisi ya Uhamasishaji, Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) Erick Ketagory (wa kwanza kulia) akiwa na afisa habari wa Taasisi hiyo Godwin Masabala 9wa pili kulia) wakizungumza na wageni waliotembelea kwenye banda lao kufahamu jinsi taasisi hiyo inavyotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.


Na: Mwandishi wetu Dar.


Afisa Mawasiliano wa Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) Godwin Masabala amesema kuwa Taasisi hiyo imedhamiria kutoa elimu kwa wananchi ili kuwajengea uelewa wa namna inavyotimiza majukumu yake ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini,Mafuta na Gesi Asilia kwa mujibu wa Sheria.


Ameyataja majukumu yao wanayoyasimamia kwa mujibu wa sheria ni pamoja na kuweka wazi taarifa za Mapato ya Serikali na malipo ya Kodi yanayotoka kwenye Kampuni za Madini,Mafuta na Gesi Asilia kwa Umma ili kuhamasisha Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali hizo.


Masabala ameyasema hayo katika mahojiano maalum na waandishi wa habari yaliyofanyika Julai 11,2022 katika Banda lao lililopo ndani ya Banda kuu la STAMICO kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.


Amefafanua kua Taasisi hiyo imeundwa kwa Sheria namba 23 ya TEITA ya mwaka 2015 ambayo imeunda Kamati ya Uwazi na Uwajibikaji (Kamati ya TEITI) yenye wajumbe nane(8) na inaongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu Ludovick Utouh na kazi za kila siku za TEITI zinatekelezwa na Katibu Mtendaji.


"Taasisi hii ina wajibu mkubwa wa kuhamasisha Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini,Mafuta na Gesi Asilia" amefafanua.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments