HATIMAYE MWILI WA MAREHEMU ULIOHIFADHIWA MOCHWARI MIAKA 6 WAZIKWAFamilia moja mjini Kisii nchini Kenya sasa inaweza kupumua baada ya kumzika jamaa yao ambaye amekuwa katika chumba cha kuhifadhi maiti kwa zaidi ya miaka sita iliyopita.

Tangu 2017, familia ya Mzee Joseph Abuga Oribo imekuwa katika majonzi tokea mwanao alipofariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Lakini mipango ya maziko ilisitishwa kufuatia zuio la mahakama kuhusu mzozo wa ardhi ya ekari tatu ambayo haukuwa umetatuliwa.

Hali ilizidi kuwa mbaya baada ya mjukuu wa marehemu pia kuugua katika hospitali ya Keroka na hatimaye kuaga dunia.

Mwili wa mjukuu huyo pia ulizuiliwa kwa zaidi ya miezi mitatu huku kukiwa na mkwamo katika shughuli za mazishi na ilibidi Waziri wa Mambo ya Ndani Fred Matiangi kuingilia kati ili mwili huo kuachiliwa na kufanyiwa mazishi.

Mjane Dinah Moraa alieleza furaha yake kuona mume wake mwenye umri wa miaka 85 pamoja na mjukuu huyo wakizikwa nyumbani kwao katika Kijiji cha Iranya Nyamache.

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post