DKT. MAGEMBE ATOA SIKU MBILI KUWASILISHA TAARIFA YA UKAGUZI WA BIDHAA ZA TIBA


Naibu  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Afya), Dkt. Grace Magembe ametoa siku mbili kwa Mganga Mkuu wa hospitali ya  Mtwara kuwasilisha  taarifa ya ukaguzi wa dawa , vitendanishi pamoja na vifaa tiba  katika  Kituo cha Afya cha Ufukoni kilichopo katika Manispaa ya Mtwara Mikindani.

 Agizo hilo limetolewa tarehe 26 Julai,  baada ya  Dkt. Magembe kutembelea kituo hicho na kubaini mapungufu  katika leja za mapokezi na matumizi ya dawa , vifaa tiba na vitendanishi vya maabara.

Pia amemtaka kushirikiana na mkaguzi wa ndani wa  Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani katika kutekeleza ukaguzi huo.

“ Haiwezekani  dawa zitumike bila rekodi, TAMISEMI ilishatoa maelekezo na nyenzo ya  ukaguzi wa dawa, vifaa tiba na  vitendanishi, ni swala la utekelezaji tu,” amesema Dkt. Magembe

Pia amewaekekeza  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara  na wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara kufanya mabadiliko ya uongozi katika  Kituo cha Afya Ufukoni ikiwemo kumpangia majukumu mengine Mganga Mfawidhi wa kituo hicho. 

Aidha, Dkt. Magembe ametumia fursa hiyo kuwahimiza Wakurugenzi wa Halmashauri za Mtwara na Nanyamba kuongeza kasi ya ujenzi unaoendelea katika Hospitali za Halmashauri.

Pia amewataka kuhakikisha wanatenga fedha za kumalizia kazi kwa  haraka na ubora ili huduma zianze kutolewa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post