NGUVU YA AMCOS YAANZA KUONEKANA, KISHAPU NA CHATO WAKO MOTO SANAMuonekano wa mafuta yaliyosindikwa katika Kiwanda cha Ushirika wa Kilimo na Masoko Chato cha kusindika mafuta ya alizeti (Chato AMCOS Sunflower Oil double refining factory) cha chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) Chato. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Mhandisi wa Kiwanda cha Ushirika wa Kilimo na Masoko Chato cha kusindika mafuta ya alizeti (Chato AMCOS Sunflower Oil double refining factory) cha chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) Chato, Mashaka Missana akionesha mafuta yalisindikwa katika kiwanda hicho.
             

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 

Baada ya Vyama Vya Msingi vya Ushirika (AMCO) vilivyokuwa vimesinzia kufufuliwa na kuanzishwa mpya kwenye mikoa kwenye mikoa inayolima zao la pamba, nguvu ya Ushirika imeanza kuonekana.

Wakitembelea Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) vinavyolima zao la pamba na alizeti wilayani Kishapu mkoani Shinyanga na Chato mkoani Geita kwa nyakati tofauti mapema wiki hii, Maafisa Mawasiliano wa Wizara ya Kilimo na Waandishi wa habari wameona nguvu ya Ushirika inavyoweza kubadilisha mbinu za uzalishaji na kuchangia maendeleo ya uchumi wa mtu mmoja na nchi kwa ujumla.

 

Wakiwa katika Chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) Kishapu mkoani Shinyanga, wamekutana na Trekta ambayo imenunuliwa na AMCOS hiyo kwa fedha taslimu Milioni 35 ambazo zimetokana na kiasi cha shilingi milioni 15 walizopewa mkopo na Benki ya NMB kwa riba ya asilimia 9% mkopo ambao watarejesha ndani ya miaka mitatu, jambo ambalo wamesema liko ndani ya uwezo wao.


“Trekta hili litasaidia kuongeza uzalishaji kwa wanachama wetu, pia tutawalimia wakulima wengine hivyo tutaongeza uzalishaji wa zao la pamba na mazao mengine”,alisema Mwenyekiti wa Kishapu AMCOS, Emmanuel Sona.


“Tumefanikiwa pia kudhibiti ubora wa pamba ambapo sasa wakulima wameachana na tabia ya kuchafua pamba kwa kuongeza mawe, maji na mchanga na vitu vingine. Tunashukuru bei ya pamba iko vizuri na haijashuka kwenye bei elekezi ya serikali shilingi 1560 kwa kilo moja ya pamba lakini tunaomba wanunuzi waje kununua pamba kwa bei ya ushindani”,amesema Sona.

 

Na huko mkoani Geita ,Chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) kimeanzisha Kiwanda cha Ushirika wa Kilimo na Masoko Chato cha kusindika mafuta ya alizeti (Chato AMCOS Sunflower Oil double refining factory), wamenunua lori la mizigo, trekta na kujenga ghala la kuhifadhia nafaka kutokana na ushuru walizokusanya na mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB).


“Ununuzi wa zana hizi za kilimo umeongeza uzalishaji na kuwapa wananchi unafuu wa upatikanaji wa mafuta,kulimiwa mashamba na kusomba mizigo pamoja ajira”, alisema Katibu wa Chato AMCOS Daudi Mahelule.

Mhandisi wa  Kiwanda cha Ushirika wa Kilimo na Masoko Chato cha kusindika mafuta ya alizeti (Chato AMCOS Sunflower Oil double refining factory) cha chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) Chato, Mashaka Missana akionesha mitambo ya kusindika mafuta katika kiwanda hicho. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mhandisi wa  Kiwanda cha Ushirika wa Kilimo na Masoko Chato cha kusindika mafuta ya alizeti (Chato AMCOS Sunflower Oil double refining factory) cha chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) Chato, Mashaka Missana akionesha mitambo ya kusindika mafuta katika kiwanda hicho
Muonekano wa sehemu ya mitambo katika Kiwanda cha Ushirika wa Kilimo na Masoko Chato cha kusindika mafuta ya alizeti (Chato AMCOS Sunflower Oil double refining factory) cha chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) Chato.
Muonekano wa sehemu ya mitambo katika Kiwanda cha Ushirika wa Kilimo na Masoko Chato cha kusindika mafuta ya alizeti (Chato AMCOS Sunflower Oil double refining factory) cha chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) Chato.
Muonekano wa sehemu ya mitambo katika Kiwanda cha Ushirika wa Kilimo na Masoko Chato cha kusindika mafuta ya alizeti (Chato AMCOS Sunflower Oil double refining factory) cha chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) Chato.
Muonekano wa mafuta yaliyosindikwa katika Kiwanda cha Ushirika wa Kilimo na Masoko Chato cha kusindika mafuta ya alizeti (Chato AMCOS Sunflower Oil double refining factory) cha chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) Chato.
Katibu wa Chato AMCOS Daudi Mahelule akionesha trekta ya chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) Chato.
Maandishi katika chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) Chato
Mkuu wa Idara ya Kilimo , Ushirika na Umwagiliaji wilaya ya Kishapu (Afisa Ugani) akielezea kuhusu trekta lililonunuliwa na Chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) Kishapu
Mkuu wa Idara ya Kilimo , Ushirika na Umwagiliaji wilaya ya Kishapu (Afisa Ugani) akielezea kuhusu trekta lililonunuliwa na Chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) Kishapu
Mwenyekiti wa Chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) Kishapu, Emmanuel Sona akielezea kuhusu namna walivyojipanga kwenye kilimo cha pamba wilayani Kishapu
Zoezi la kununua pamba ya wakulima likiendelea katika Chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) Kishapu
Zoezi la kununua pamba ya wakulima likiendelea katika Chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) Kishapu.
Muonekano sehemu ya pamba iliyopo katika ghala la Chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) Kishapu.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments