WAHUNI WAVAMIA KANISA ASKOFU AKIENDELEA KUHUBIRI...WAPORA VITO VYA THAMANI

Mhubiri anayejulikana kwa mtindo wake wa maisha ya ufahari ameibiwa vito vya thamani ya zaidi ya $1m (£840,000) wakati wa mahubiri yaliyopeperushwa moja kwa moja katika jiji la New York.

Lamor Whitehead, 44, ameapa kwamba wahalifu "hawataepuka"

Miongoni mwa vitu alivyoibiwa, mhubiri huyo anayeendesha gari aine ya Rolls Royce ni saa aina ya Rolexes, almasi na zumaridi.

Polisi bado wanachunguza tukio hilo. Mpaka sasa hakuna mshukiwa ambaye ametajwa wala kukamatwa.

Katika video hiyo Bw Whitehead anasikika akiuliza "Ni wangapi kati yenu mmepoteza imani kwa sababu mliona mtu mwingine akifa?" muda mfupi kabla ya watu kadhaa waliovalia nguo nyeusi kuingia kanisani huko Brooklyn.

"Nilipowaona wakiingia kwenye hekalu na bunduki zao, nilimwambia kila mtu [alale] chini, kila mtu alale," baadaye alisema kwenye ukurasa wa Instagram."Sikujua kama walitaka kulipiga risasi kanisa au kama walikuwa wanakuja kwa wizi."Kulingana na Bw Whitehead, wezi hao waliojifunika nyuso zao walitoroka kwa kutumia gari aina ya Mercedes.

Kufuatia wizi huo, gazeti la New York Post liliripoti kuwa vitu vilivyochukuliwa kutoka kwake na mkewe ni pamoja na saa za Rolex na Cavalier za $75,000, rubi ​​ya Episcopal ya $25,000 na pete ya almasi na pete za $25,000 - na hata pete yake ya harusi.

BBC imewasiliana na Bw Whitehead ili kupata maoni yake.

Katika taarifa, meya wa jiji la New York Eric Adams - ambaye amemfahamu Bw Whitehead tangu mwaka 2013 - alisema kuwa Idara ya Polisi ya New York ilikuwa ikichunguza uhalifu huo.

"Hakuna mtu katika jiji hili anayepaswa kuwa muathiriwawa wizi wa kutumia silaha, achilia mbali viongozi wetu wa kidini," Bw Adams alisema.

Bw Whitehead, kwa upande wake, ametoa zawadi ya dola 50,000 kwa atakayetoa habari zitakazowezesha kukamatwa.

Tukio la hivi punde, hata hivyo, lilizua ukosoaji mwingi kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kupenda anasa na maisha ya kifahari.

Chanzo - BBC Swahili

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments