WAUAWA KWA WIVU WA MAPENZI DODOMA


Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Dodoma, ACP Martini Otieno
**
Watu wawili wameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali katika mtaa wa Msangalale, Kata ya Dodoma Makulu jijini Dodoma huku wivu wa mapenzi ukitajwa kuwa chanzo cha vifo hivyo.


Waliouawa ni Dominick Kigula ambaye ni dereva wa pikipiki (Bodaboda) na mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Esta

Mganga mkuu wa Hospitali ya mkoa wa Dodoma, Ibenze Ernest, amesema miili ya waliowawa imepokelewa na kuhifadhiwa hospitalini hapo.

Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Dodoma, ACP Martini Otieno, amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo huku akisema wanaendelea na jitahada za kumpata mtuhumiwa.

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post