MREMBO AAMUA KUFUNGA NDOA KUJIOA MWENYEWE


Kshama Bindu mwanamke aliyejioa mwenyewe

MWANAMKE mmoja anayefahamika kwa jina la Kshama Bindu raia wa India mwenye umri wa miaka 24 amekuwa gumzo mitandaoni baada ya kufunga ndoa ya kujioa yeye mwenyewe.


Harusi ya Bindu ilifanyika June 8 mwaka huu katika mfumo mpya wa harusi za tamaduni za watu wa India ambapo ameweka rekodiya kuwa mwanamke wa kwanza kufunga ndoa ya aina hiyo.


Bindu amesema alikuja na wazo lakujioa yeye mwenyewe ikiwa nimiezi mitatu imepita tangu alipoona mchezo kutoka Netflix unaofahamika kama Anne with AN E, mchezo uliomuonesha motto yatima ambaye alikumbwa na kadhia ya ubaguzi na unyanyasaji wa kijinsia tangu akiwa mdogo.


“Nataka kuwa muoaji na siyo mke.” Hatimaye mnamo Juni 8, akafanikiwa kujioa mwenyewe.

Kshama Bindu amesema kwa kujioa mwenyewe anaweza kupata uhuru wa kuzuru sehemu yoyoteile aitakayo

Tangu kipindi hicho Bindu amepata wakati mgumu wakati akiwa anasafiri katika shughuli zake za kazini au katika manunuzi ya bidhaa magharibi mwa mji wa Gujarat ambapo amekuwa akiangaliwa kama mtu asiyekuwa wa kawaida na baadhi ya watu katika mji huo.


Aidha Kshama Bindu amebainisha kuwa moja ya faida anayoipata ni kwamba atakuwa huru kuzuru sehemu yoyote ile aitakayo bila kuhitaji kibali cha mtu mwingine au kuwaza kuhusu mtu mwingine kuhamisha makazi kwa sababu yake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

1/Post a Comment/Comments

Post a Comment