KINANA AWASILI KATAVI KWA ZIARA YA KIKAZI, KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO


Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulrahman Kinana akiwa katika picha mbalimbali akisaliamia na wana CCM mkoa wa Katavi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Katavi kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi sambamba na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho.PICHA NA MICHUZI JR-KATAVI


**

Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Katavi

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana amewasili mkoani Katavi kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi itakayokwenda sambambamba na kupokea taarifa na kukagua miradi ya maendeleo.

Katika ziara hiyo ya kikazi ameongazana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Shaka Hamdu Shaka na baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege Katavi Kinana amepokelewa na Wana CCM Mkoa wa Katavi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Mkoa Beda Katani.

Baada ya kuwasili Kinana akiwa na Shaka wamepata nafasi ya kusailiamana na wanachama wa Chama hicho na kisha kupokea taarifa ya CCM na Serikali Mkoa wa Katavi.

Akipokea taarifa hiyo Kinana ameelezwa hali ya mwenendo wa Chama na Serikali na kwa sehemu kubwa ameambiwa hali ni shwari na kwamba viongozi wamekuwa na ushirikiano mkubwa hali inayofanywa utekelezaji wa Ilani kufanyika kwa kiwango cha kuridhisha.

Kwa mujibu wa ratiba Kinana ambaye ameanza ziara leo Julai 25 ,2022 akiwa mkoani hapa mbali ya kupokea taarifa ya Chama na Serikali atazindua mradi wa fremu 15 za biashara, pia atatembelea mradi wa fremu za vibanda 188.

Aidha Kinana atazindua kituo cha afya na kuzungumza na wananchi na wanachama, pia baadae atazungumza na WanaCCM na viongozi mbalimbali . Kinana atakuwa katika ziara ya mikoa ya Nyanda za Juu ukiwemo Mkoa wa Katavi na kisha kuelekea Mkoa Rukwa, Songwe na Mbeya.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Abdulrahaman Kinana akisailiamiana na viongozi wa Chama na Serikali mkoa wa Katavi baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Mpanda kwa ajil ya kuanza ziara mkoani humo
Matukio mbalimbali katika picha baada ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Abdulrahman Kinana kuwasili uwanja wa ndege wa Mpanda mkoani Katavi kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Ndugu Abdulrahman Kinana akisaliamiana na viongozi wa Chama na Serikali Mkoa wa Katavi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege Mpanda kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments