WAFANYAKAZI WIZARA YA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI WATAKIWA KUCHAMBUA FURSA ZA KIUCHUMI KUSAIDIA KUFUNGUA AJIRA ZA KIMATAIFA


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Tehama Dkt.Jimmy Yonaz akiongea kwenye kikao kazi cha uchambuzi wa fursa za kiuchumi za sekta ya mawasiliano Kitaifa na Kimataifa kinachokusudia kufungua ajira.
Baadhi ya Habari, mawasiliano na teknolojia ya Habari imefanya kikao kazi cha uchambuzi wa fursa za kiuchumi za sekta ya mawasiliano Kitaifa na Kimataifa huku ikiwa imekusudia kufungua ajira


Na Dotto Kwilasa,DODOMA.
WIZARA ya Habari, mawasiliano na teknolojia ya Habari imefanya kikao kazi cha uchambuzi wa fursa za kiuchumi za sekta ya mawasiliano Kitaifa na Kimataifa huku ikiwa imekusudia kufungua ajira kwa watanzania kitaifa na kimataifa .


Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.Jimmy Yonazi ametumia nafasi hiyo kuwataka wafanyakazi wa sekta ya mawasiliano nchini kukuza maarifa na kuwa na uchumi shindani wa kidijitali ili kuwa kitovu cha watu kujifunza namna ya kutafuta fursa katika taasisi za kimataifa.
The
Akiongea kwenye kikao hicho jana Jijini hapa,Dkt.Yonazi alisema Wizara hiyo itatumia vikao vya mara kwa mara vitakavyo chambua fursa za kiuchumi za sekta ya mawasiliano ili kuwa na nchi yenye fursa nyingi kiasi ambacho nchi zingine zitaweza kujifunza.


"Ili kuifanya Tanzania kuwa nchi ya fursa lazima kila mfanyakazi wa sekta hii aielewe sekta hiyo na mifumo yake,kila mmoja atambue jukumu lake na siyo kuja ofisini na kurudi nyumbani tu,"alisema na kuongeza;


Kwa mfano sasa hivi tunaelekea kwenye suala la sensa na tunaenda kutumia vishikwambi na vitahitajika vingi tusipojua mapema wapi tutavipata tutaenda kule China tutaangaika kwenye makampuni yanayotengeneza huku muda ukiwa umeisha hatutapata vyenye ubora hivyo tujitahidi kujua mapema mahitaji yetu ,"alisema.


Vile vile aliwataka wafanyakazi wa Wizara hiyo kuifahamu wizara hiyo na kazi zake Ili kuwavutia watu wengine na kwamba kama kuna mtu anataka kujifunza basi aende kujifunza katika wizara hiyo jinsi ya kutumia fursa za nje ya nchi.


Naye Mkurugenzi wa TEHAMA Wizara ya Habari, mawasiliano na teknolojia ya Habari, Mulembwa Munaku alisema kuwa watatekeleza maagizo ya serikali ili kuongza ajira pamoja na pato la Taifa.


Alisema lengo ni kuifanya Wizara hiyo kuwa imara iliyosambaa nchini kote Kutokana na wataalam waliobobea na wenye uwezo wa kutoa huduma ya mawasiliano na habari zilizo sahihi na zenye kuaminika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments