UPANUZI WA KIWANDA CHA LABIOFAM KUSAIDIA UZALISHAJI WA MBOLEA NCHINI

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe Dkt.Ashatu Kijaji (Mb.) akizungumza na ugeni kutoka nchini Cuba ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Mhe. Bruno Rodriguez Parrilla ambapo wamefanya majadiliano kuhusu uwezekano wa kupanua zaidi kiwanda cha kuzalisha viwatilifu ili kuzalisha bidhaa ya mbolea pamoja na bidhaa zingine za Afya. Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe Dkt.Ashatu Kijaji (Mb.) akizungumza na ugeni kutoka nchini Cuba ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Mhe. Bruno Rodriguez Parrilla ambapo wamefanya majadiliano kuhusu uwezekano wa kupanua zaidi kiwanda cha kuzalisha viwatilifu ili kuzalisha bidhaa ya mbolea pamoja na bidhaa zingine za Afya. Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe Dkt.Ashatu Kijaji (kulia) akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Mhe. Bruno Rodriguez Parrilla mara baada ya kukutana kufanya mazungumzo leo Juni 30,2022 katika Ofisi za kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe Dkt.Ashatu Kijaji (kulia) akizungumza jambo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Mhe. Bruno Rodriguez Parrilla mara baada ya kukutana kufanya mazungumzo leo Juni 30,2022 katika Ofisi za kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe Dkt.Ashatu Kijaji akipata picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Mhe. Bruno Rodriguez Parrilla mara baada ya kukutana kufanya mazungumzo leo Juni 30,2022 katika Ofisi za kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Mhe. Bruno Rodriguez Parrilla (kushoto) akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Mhe. Valentino Mlowola mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo leo Juni 30,2022 katika Ofisi za kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe Dkt.Ashatu Kijaji (Mb.) leo Juni 30,2022 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Mhe. Bruno Rodriguez Parrilla ambapo wamefanya majadiliano kuhusu uwezekano wa kupanua zaidi kiwanda cha kuzalisha viwatilifu ili kuzalisha bidhaa ya mbolea pamoja na bidhaa zingine za Afya.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Waziri Kijaji amesema moja ya bidhaa ambayo wanataka kuzalisha kwenye kiwanda cha Labiofam kilichopo Kibaha mkoani Pwani ni mbolea ambayo itatuwezesha kuwa na utoshelevu wa mbolea ndani ya Taifa letu.

"Kilimo ni sekta ambayo inachangia kwa kiwango kikubwa kwenye uchummi wa Taifa letu hivyo mbolea ni moja ya ya malighafi muhimu kuhakikisha kilimo kinakuwa na mchango mkubwa kwenye uchhumi wa Taifa letu, sisi kama Wizara tukko tayari kuhakikisha kiwanda chetu kinaendelea na uuzalishaji wa bidhaa hizi muhimu kwaajili ya maendeleo ya Taifa letu". Amesema Waziri Kijaji.

Aidha Waziri Kijaji amesema walikuwa wamekwama katikati kupata certification ya uzalishaji wa bidhaa hizo zingine na kulikuwa na mambo walikuwa wanatakiwa kuanza majadiliano kati ya serikali ya Tanzania na Cuba hivyo waliunda timu za majadiliano kwa nchi zote mbili ambapo sasa wapo tayari kujadili kuhusu majadiliano yanayokuja kati ya wataalamu wetu kwani wanatarajia wataalamu kutoka cuba kuingia hapa nchini kuanzia Julai 8 hadi 10 kwaajili ya kuendelea na majadiliano hayo.

Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Mhe. Valentino Mlowola amesema manufaa ya ugeni kutoka nchini Cuba utasaidia kupanua ushirikiano na kujenga maeneo makubwa zaidi na uwezekano wa kutoa ajira kutokana na uwekezaji ambao wataufanya kushirikiana na Tanzaniapamoja na kupata faida za kibiashara zaidi.

"Uhusiano wetu na Cuba ni mzuri na unaendelea kuimarika siku hadi siku na wataendelea kushirikiana kwenye sekta mbalimbali hususani kwenye sekta yya afya,Elimu pamoja na Viwanda". Amesema Balozi Mlowola

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments