DAWA YA KUKAMATA WEZI YAZUA BALAA MJINI MASWA....WALIODAKWA WATAFUNA MAJANI KAMA NG'OMBE, WALA MCHANGA NA TAKATAKA

 

Na Samwel Mwanga - Maswa

*****
Watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni wezi wa vitu mbalimbali katika mji wa Maswa mkoani Simiyu wamekumbwa na hali ya kula majani kama wanyama,kula mchanga na takataka  mara baada  ya mganga wa kienyeji kutoka mkoani Mara kwa  kushirikiana na familia iliyoibiwa vitu mbalimbali Mei 29 mwaka huu,kufanya dawa hiyo.


Tukio hilo la aina yake limetokea  leo Jumapili  Juni 5 Mwaka huu, ambapo lengo kuu la kumuita mganga huyo, ilikuwa ni kuwarudisha watu waliomuiba  magodoro mawili,,Radio aina  ya Subwoofer,Viazi mviringo kg 20 na sufuria iliyokuwa na nyama ya ng'ombe iliyopikwa.


Wizi katika mji huo umekithiri kwa matukio ya watu mbalimbali kuibiwa vitu mbalimbali wakiwemo na kuku kwa kuvunja madirisha na milango kwenye nyumba nyakati za usiku na mchana.


Imeelezwa kuwa mara baada ya dawa hiyo kufanyika ambapo  mhusika,Mantesa Lukumba ambaye ni mkazi wa Maswa  alileta mganga ili kuwabaini wahusika na kuwashirikisha watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa kitongoji wa Majengo mahali anapoishi.


Hivyo kila mmoja wakiwemo vijana hao waliombwa kunywa dawa ya mganga huyo au kuacha maana ni hiyari hivyo watu walio wengi waliamua kunywa na vijana hao  walirudi na kuanza kukata majani na kuyala kama wafanyavyo Ng'ombe,kula mchanga na takataka kitendo ambacho wamekifanya wakiwa kwenye hali ya kutojitambua, huku wakishuhudiwa na Umati wa watu waliokusanyika kwenye nyumba hiyo.


Baadaye askari polisi walifika majira ya saa 1:40 jioni na kuwachukua na kuwapeleka kituo cha polisi kwa ajili ya usalama wao lakini imeelezwa kuwa hadi watakaporejesha kiasi cha fedha kila mmoja Sh 800,000 kufidia gharama za thamani ya vitu walivyoiba ndipo watakaporudishwa kwenye hali yao ya kawaida.


Kwa upande wake  aliyeibiwa Mantesa , ameeleza ni kwa namna gani alibaini kuwa ameibiwa alisema kuwa wezi hao waliruka ukuta usiku wakiwa wamelala  wakavunja dirisha na kukata nondo na kufanikiwa kuiba vitu hivyo ambavyo hadi sasa havijapatikana  kwahiyo msaada mbadala ndiyo tulioutumia na ndiyo hiki mnachokiona.

Tazama video hapa

Tazama Wezi wakila majani kama wanyama Maswa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

1/Post a Comment/Comments

  1. Waliokamatwa kwa njia ya ushirikina Maswa

    ReplyDelete

Post a Comment