UWT SHINYANGA WAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA UTENDAJI WAKE KATIKA KUWAHUDUMIA WANANCHI


Umoja wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Cha Mapinduzi (Ccm) Mkoa wa Shinyanga umefanya Kikao cha wajumbe wake wa Kamati kwa Lengo la Kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan kwa utendaji wake katika kuwahudumia Wananchi .


Akizungumza wakati wa kutoa Pongezi hizo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza hilo Mheshimiwa Sophia Mjema amesema wanatambua mchango ambao unatolewa na Rais ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mama Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha umoja wa Wanawake Tanzania unakuwa imara, mshikamano na upendo wakati wote.


Mhe. Mjema ameongeza kuwa yeye kama Mkuu wa Mkoa ambaye anamuwakilisha Mhe.Mama Samia katika kuhakikisha anamsaidia vyema kuusimamia Mkoa pamoja na kusimamia Fedha anazozitoa kwa ajili Maendeleo ya pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitatua.


Katibu wa Umoja wa Wanawake Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga Bi. Asha Juma amesema agenda Kuu ni kumpongeza Rais Samia kwa utendaji wake na jinsi anavyowahudumia Wananchi kwa ustadi na weledi mkubwa hasa kwa mambo makubwa ambayo ameyafanya kwa Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni pamoja na kiasi cha Fedha alichotoa kwa ajili ya shughuli za Maendeleo kwa kila Halmashauri ndani ya mwaka mmoja toka ameingia madarakani.


Bi. Asha Juma ameongeza kuwa Mama Samia ameweza kumtua Mwanamke ndoo kichwani kwa kuongeza upatikanaji kwa urahisi wa Maji katika Mkoa wa Shinyanga.


Aidha ameongeza kuwa Mhe. Samia ameweza kufanikisha Ujenzi wa Shule za Msingi, Sekondari,Vyuo na Vyuo vya ufundi stadi(Veta) ambapo Itasaidia kuhakikisha kila mtoto wa kitanzania anapata elimu iliyo bora .


Rais Samia ameweza kufanya uteuzi wa nafasi mbalimbali za wanawake katika nafasi nyeti na za juu huku akitolea mfano kwa uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dokta Sophia Mjema.


Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Bi. Magreth Cosmas amesema Baraza na Jumuiya ya Wanawake wa Ccm Taifa na Mikoa yote wanaungana na Mwenyekiti wao Kitaifa katika kutambua mchango mkubwa unaotolewa katika kuiletea Tanzania Maendeleo kuanzia kwa Wananchi wake na Kulitangaza Taifa kiujumla.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post