CHUO CHA AFYA KOLANDOTO,KISIMA CHA UBOBEZI TAALUMA YA UFAMASIA ,UTABIBU,UUGUZI KATIKA SOKO LA AJIRA




Mkuu wa Idara ya Famasia Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga ,Paschal Marusu,akitoa maelezo kwa wananchi kuhusu Kozi zinazotolewa na chuo hicho waliotembelea Banda la Chuo hicho wakati Maonyesho ya Elimu ya Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Stadi TVET,yaliyomalizika leo Juni 13,2022 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma


MWANAFUNZI Kozi ya Famasi mwaka wa pili Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Rahma Khamis,akiwaonyesha dawa wananchi zinazotengezewa katika chuo hicho waliotembelea Banda la Chuo hicho wakati Maonyesho ya Elimu ya Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Stadi TVET,yaliyomalizika leo Juni 13,2022 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.


MWANAFUNZI Kozi ya Famasi mwaka wa pili Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Thobias Vitus,akizungumza na wananchi waliotembelea Banda la Chuo hicho wakati Maonyesho ya Elimu ya Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Stadi TVET,yaliyomalizika leo Juni 13,2022 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.


Msanii wa muziki Bongo, Banana Zorro,akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea Banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga wakati Maonyesho ya Elimu ya Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Stadi TVET,yaliyomalizika leo Juni 13,2022 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.


MWANAFUNZI Kozi ya Uuguzi na Ukunga Famasi mwaka wa tatu Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Elizabeth Daudi,akimueleza Msanii wa muziki Bongo, Banana Zorro,jinsi wanavyomzalisha Mama Mjamzito mara baada ya kutembelea Banda la Chuo hicho wakati Maonyesho ya Elimu ya Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Stadi TVET,yaliyomalizika leo Juni 13,2022 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.


MWANAFUNZI Kozi ya Uuguzi na Ukunga Famasi mwaka wa tatu Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Elizabeth Daudi,akiwaelezea kwa vitendo wananchi jinsi wanavyomsaidia Mama Mjamzito kujifungua mara baada ya kutembelea Banda la Chuo hicho wakati Maonyesho ya Elimu ya Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Stadi TVET,yaliyomalizika leo Juni 13,2022 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.


Mkuu wa Idara ya Famasia Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga ,Paschal Marusu,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye Banda la Chuo hicho wakati Maonyesho ya Elimu ya Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Stadi TVET,yaliyomalizika leo Juni 13,2022 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma


Mkuu wa Idara ya Famasia Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga ,Paschal Marusu,aakionyesha dawa zinazozalishwa katika chuo hicho kwenye Banda la Chuo hicho wakati Maonyesho ya Elimu ya Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Stadi TVET,yaliyomalizika leo Juni 13,2022 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma


Mwalimu Idara ya Uuguzi Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga,Peris Nderitu,akielezea huduma zinazotolewa katika chuo hicho na namna ya kumzalisha mama mjamzito kwenye Banda la Chuo hicho wakati Maonyesho ya Elimu ya Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Stadi TVET,yaliyomalizika leo Juni 13,2022 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.


Picha ya pamoja

………………………………………

Na.Alex Sonna-Dodoma.

Mkuu wa Idara ya Famasia Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga ,Paschal Marusu ametoa wito kwa vijana kuchangamkia fursa za kujiunga na masomo yanayotolewa katika chuo hicho ili kuongeza ujuzi na kupanua wigo wa kujiajiri ama kuajiria katika sekta za afya.

Hayo ameyasema wakati wakati Maonyesho ya Elimu ya Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Stadi TVET,yaliyomalizika leo Juni 13,2022 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma

Bw.Marusu amesema jkuwa katika chuo hicho kinatoa mafunzo mbalimbali ya ufundi pamoja na afya ikiwemo,utabibu,uuguzi na famasia na maabara hivyo kuna fursa kubwa kwa vijana kujiunga na chuo hicho katika kuongeza wigo wa taaluma sekta ya afya.

“Katika chuo chetu kuna program mbalimbali ikiwemo program ya utabibu,program ya uuguzi ambayo ni ya muda mrefu ina Zaidi ya miaka 60,pia tuna program ya maabara ya binadamu na katika chuo chetu tumekuwa tukifundisha kwa vitendo Zaidi na hapa tumeleta baadhi ya dawa ambazo hutengenezwa “amesema Bw.Marusu

Aidha,amesema katika program ya uuguzi wamekuwa na vifaa madhubuti ikiwemo baadhi ya vifaa vinavyoonesha namna ya kumsaidia mama anayejifungua.

Mbali na mafunzo ya afya yanayotolewa katika chuo hicho pia kina masomo yanayohusiana na mafunzo ya ufundi stadi (VETA).

Kwa upande wake Mwalimu Idara ya Uuguzi Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga,Peris Nderitu,amesema kuwa huduma zinazotolewa katika chuo hicho zimekuwa na manufaa makubwa kwa jamii ikiwemo namna ya kumzalisha mama mjamzito.

“Tunatoa mafunzo kwa vitendo kwa v mfano namna ya kumhudumia mama anapojifungua,pia dawa gani atumie na dawa zipi asitumie nahii yote ni katika kuhakikisha viwango vya vifo kwa akina mama na watoto vinapungua”amesema Mwl Nderitu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments