RAIS SAMIA ASHUHUDIA UWEKAJI SAINI MIKATABA YA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA MBALIMBALI KATI YA TANZANIA NA OMAN


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimshuhudia Waziri wa Nishati January Makamba wakati akiweka Saini Mkataba wa Makubaliano kwenye masuala ya Nishati (Oil and Gas) kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Oman kupitia Wizara ya Nishati na Madini (Sekta ya Madini) ya nchi hiyo katika hafla iliyofanyika Al Bustan, Muscat nchini Oman tarehe 13 Juni, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimshuhudia Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akiweka Saini Mkataba wa Makubaliano kwenye Sekta ya Elimu ya Juu pamoja na Serikali ya Oman katika hafla iliyofanyika Al Bustan, Muscat nchini Oman tarehe 13 Juni, 2022.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) Shariff Ali Shariff akisaini Mkataba wa Makubaliano pamoja na Mamlaka ya kukuza Uwekezaji Oman (OIA) kuhusu Mashirikiano ya kutangaza Uwekezaji baina ya nchi mbili kushirikiana katika kupata uzoefu na kusaidiana katika uwezeshaji wa kiteknolojia na Mafunzo iliyowakilishwa Naibu Mtendaji Mkuu wa (OIA) Mulham Basheer Al Jaraf tarehe 13 Juni, 2022.

Mkataba wa Makubaliano katika ya Jumuiya ya Watoa huduma katika Sekta ya mafuta na Gesi (AGAS) na Jumuiya ya watoa huduma katika sekta ya mafuta na gesi Zanzibar ZAOGAS pamoja na Jumuiya ya watoa huduma za Mafuta kutoka Oman (OPAL) katika hafla iliyofanyika Muscat Oman Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya Biashara ya Zanzibar Ali Amour katikati ni Mwenyekiti wa ATOG Balozi Abdulsamad Abdulrahim na kwa upande wa Oman ni Mkurugenzi Mtendaji wa OPAL Abdulrahman Al Yahya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post