KIJANA AKAMATWA KWA MAMA JOHN AKITAPELI KWA KUJIFANYA MKUU WA MKOAJeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Warren Max Mwinuka (20) Mkazi wa Makondeko – Mbeya Mjini kwa tuhuma za kujifanya Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera akitumia akaunti ya mtandao wa kijamii wa Instagram kwa jina la “juma_homera”.

Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 07.06.2022 majira ya saa 08:00 mchana huko maeneo ya Mama John Jijini Mbeya. Mtuhumiwa alikuwa akitumia akaunti hiyo kuwaadaa watu kwa kujifanya ni Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na kutoa namba ya simu yak wake ili wananchi waweze kutoa/kupeleka kero/shida mbalimbali kwake. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika atafikishwa mahakamani.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments