WANANCHI KASULU WALALAMIKIA MASOKO YA USIKU CHANZO TABIA MBAYA KWA WATOTO


Mratibu wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) Flora Ndaba akizungumza katika mdahalo wa kupambana na ukatili wa kijinsia ulioandaliwa na shirika hilo kwa wananchi wa kijiji cha Murufiti Halmashauri ya mji wa Kasulu mkoani Kigoma.
Mratibu wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) Flora Ndaba akizungumza katika mdahalo wa kupambana na ukatili wa kijinsia ulioandaliwa na shirika hilo kwa wananchi wa kijiji cha Murufiti Halmashauri ya mji wa Kasulu mkoani Kigoma.
Katarina Kakunze Mwananchi kutoka kijiji cha Titye Halmashauri ya wilaya Kasulu akizungumza kwenye mdahalo wakupinga ukatili wa kijinsia kwenye kijiji hicho ulioandaliwa na Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP).
Adolf Kilambi Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Titye halmashauri ya wilaya Kasulu akizungumza katika mdahalo wa kupinga ukatili wa kijinsia ulioandaliwa na Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) na kufanyika kwenye kijiji cha Titye wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.


**

Na Fadhili Abdallah,Kigoma


WANANCHI wa vijiji vya TITYE na Murufiti wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wamesema kuwa masoko ya usiku bado ni changamoto kubwa katika kukabili mimba za utotoni na tabia mbaya za watoto licha ya wananchi hao kupiga kelele kwa muda mrefu.

Wakizungumza kwa nayakati tofauti katika midahalo iliyokuwa ikiendeshwa na Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) wananchi hao walisema kuwa wanaiomba serikali kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha masoko hayo hayawi chanzo cha tabia mbaya kwa watoto kupata ujauzito kupitia masoko hayo.

Mmoja wa wananchi hao, Chada Salum akizungumza kwenye mdahalo uliofanyika kwenye kijiji cha Murufiti halmashauri ya mji wa Kasulu alisema kuwa sheria kali zinapaswa kupitishwa na baraza la madiwani ili masoko hayo ya usiku yasiwe chanzo cha ukatili kwa wasichana kupata mimba zisizotarajiwa.

Naye Dafroza George kutoka kijiji cha Murufiti alisema kuwa masoko ya usiku yamekuwa na dhana mbaya ya kuitwa soko mapenzi kutokana na wasichana wengi kutumia nafasi ya kwenda kuuza au kununua mahitaji kwenye masoko hayo hivyo kujiingiza kwenye vitendo vya kufanya mapenzi na kupata ujauzito.

Kwa upande wake Meliciana Hamisi kutoka kijiji cha Titye Halmashauri ya wilaya Kasulu alisema kuwa bado masoko ya usiku ni tatizo kubwa katika kudhibiti mimba kwa wanafunzi kwani bado serikali za vijiji hazijaweza kuchukua hatua madhubuti kukabili mienendo mibaya inayotokea inayosababishwa na masoko hayo.

Akizungumzia malalamiko na tuhuma zinazotolewa na wananchi kuhusu masoko ya usiku kuwa chanzo cha mimba kwa wananfunzi na wasichana wadogo Afisa Mtendaji wa kijiji cha Titye, Ezekiel Augustino alisema kuwa serikali ya kijiji imekuwa ikichukua hatua kukabili vitendo vya ukatili kutekeleza mpango wa mtakuwa ikiwemo mimba kwa wananfunzi na wasichana wadogo, utumikswaji wa watoto na vitendo vya ubakaji na ulawiti.

Mtendaji huyo alisema kuwa wamekuwa wakitoa elimu na kuchukua hatua lakini bado wananchi wamekuwa kikwazo katika kutoa ushirikiano kudhibiti vitendo hivyo kwani watoto wanaokwenda kwenye masoko hayo wanatoka kwenye jamii ambayo leo ndiyo inayolalamika.

Mratibu wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka TGNP, Flora Ndaniye akizungumza kwa nyakati tofauti kwenye midahalo hiyo alisema kuwa bado wananchi hawana namna ya kukwepa lawama za vitendo vya ukatili na mmomonyoko wa maadili unaotokea kwenye jamii zao na mimba za utotoni kwa watoto wao.

Ndabaniye alisema kuwa kabla wananchi hawajainyooshea kidole serikali lazima watekeleza wajibu wao kwa kuhakikisha wanasimamia malezi na matunzo yenye maadili kwa watoto wao maana ndiyo wanaoishi nao kwa karibu na kwamba mashirika na mipango wanayopelekewa ni kuhamasisha utekelezaji wake tu lakini wenye jukumu la kwanza ni wananchi wenyewe wenye watoto.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments