WATU 22 WAFARIKI WAKILA BATA KLABU


Takriban watu 22, wanaume kwa wanawake, wamepatikana wamefariki dinia katika kilabu cha usiku kwenye kitongoji cha jiji la London Mashariki mwa Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchini humo, miili yao ilipatikana katika ukumbi wa Enyobeni Tavern mapema Jumapili, Juni 26, na wengine kadhaa wanasemekana kujeruhiwa. 

Msemaji wa polisi Brigedia Tembinkosi Kinana aliambia kituo cha habari cha Newzroom Africa kuwa mazingira iliyopelekea tukio hilo inachunguzwa kwa sasa.

 "Hali inayozingira tukio hilo inachunguzwa tunapozungumza. Hatutaki kufanya uvumi wowote katika hatua hii," Brigedia Tembinkosi Kinana alisema.

Kinana alisema wengi wa waliokutwa wamekufa ni vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 20. 

Kamishna wa Polisi wa Eastern Cape, Nomthetheleli Lilian Mene akizungumza na SABC News alisema kwamba kulikuwa na madai ya mkanyagano ndani ya eneo hilo la burudani. 

Lakini Unathi Binqose, afisa wa idara ya jamii na usalama ya Eastern Cape, akizungumza kutoka eneo la tukio, alipuzilia mbali mkanyagano kama chanzo cha kifo.

 "Ni vigumu kuamini kuwa ni mkanyagano kwani hakuna majeraha ya wazi yanayoonekana kwa waliofariki," Binqose aliambia shirika la habari la AFP kwa njia ya simu. 

Gazeti moja la eneo hilo, DispatchLive, liliripoti kwamba “miili imetapakaa kwenye meza, viti na sakafuni; bila dalili za wazi za kuumia”. 

Msemaji wa idara ya afya ya jimbo la Eastern Cape, Siyanda Manana, alisema miili hiyo itasafirishwa hadi katika vyumba vya kuhifadhia maiti vya serikali ambako jamaa wanatarajiwa kusaidia kuwatambua waathiriwa.

Alisema alielewa waathiriwa walikuwa wanafunzi waliokuwa wakisherehekea kumaliza kufanya mitihani wa shule ya upili.

Chanzo - Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments