AJALI YAUA WATU SITA NA KUJERUHI WANNE WAKIENDA KUZIKA TABORA


Gari iliyoua watu sita

Watu sita na wanne kati yao ni wa familia moja wamefariki dunia kwa ajali ya gari ndogo katika eneo la Inala mkoani Tabora, wakati wakitokea Dar es Salaam kuelekea wilaya ya Urambo Tabora katika mazishi ya Mama mzazi wa mmoja wa marehemu hao.


Ajali hiyo imetokea  Juni 25, 2022, majira ya jioni, ambapo kwa mujibu wa mashuhuda gari ndogo ilihama katika upande wake na kuingia kwenye uvungu wa lori lililokuwa likitokea Tabora kuelekea Singida.

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post