MKUU WA MKOA WA RUVUMA AZINDUA TAMASHA LA MAJIMAJI SELEBUKA 2022

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, ameagiza ushiriki wa wilaya na halmashauri zote za Mkoa Wa Ruvuma kwenye tamasha la Majimaji Selebuka litakalofanyika kuanzia tarehe 23 hadi 30 Julai 2022 mjini Songea. 

Tamasha hili limekuwa jukwaa kuu la biashara, kutangaza utalii, kuchochea vipaji, utamaduni , mashindano ya debate kwa shule na michezo, hivyo linatoa fursa adimu kwa mkoa wetu wa Ruvuma.


Pia mwaka huu tamasha hili litakuwa na mashindano ya baiskeli ya km 165 toka Songea hadi Mbamba Bay, mbio na mpira wa miguu na kikapu. 

Ili kuwapa urahisi washiriki kwenye Majimaji Selebuka imezindua tovuti yenye zaidi ya hoteli 200 kwa ajili wageni.

Pamoja na kutangaza vivutio vya utalii vya mkoa wa Ruvuma, Majimaji Selebuka inachochea biashara, elimu, sanaa, michezo kwenye ukanda wa kusini.


Majimaji Selebuka ni tukio linalofanyika kila mwaka Songea, Ruvuma ambapo mwaka huu litazizima kuanzia tarehe 23 hadi 30 Julai. Kujisajili ingia majimajiselebuka.co.tzDownload/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post