MWANDISHI WA HABARI WA ITV FRANK MSHANA ANUSURIKA KATIKA AJALI


Mwandishi wa habari wa ITV Mkoa wa Shinyanga Frank Mshana amepata ajali jioni hii Ijumaa Juni 17,2022 katika barabara ya Kishapu baada ya gari lake alilokuwa anasafiria kutoka Shinyanga Mjini kuelekea Kishapu kupasuka tairi na kugonga gema kisha kutumbukia kwenye korongo.

Akizungumza na Malunde 1 blog, Mshana amesema alikuwa anaelekea Kishapu kutekeleza majukumu yake ya uandishi wa habari.

"Wakati naendelea na safari yangu kuelekea Kishapu tairi ya gari yangu niliyokuwa naendesha ilipasuka, mbele kulikuwa na gari inakuja kwa mwendo kasi, kutokana na tairi kupasuka gari langu likayumba nikagonga gema kisha gari kutumbukia kwenye korongo. Namshukuru Mungu nimetoka salama japo nasikia maumivu mgongoni, gari imeharibika",amesema Mshana

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments