WAKURUGENZI WA HALMASHAURI KIGOMA WATAKIWA KUWA WABUNIFU



Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) mkoa Kigoma, Jackson Mateso akiongoza wajumbe wa ALAT kukagua miradi ya ujenzi wa majengo ya utoaji huduma kwa wananchi kwenye halmashauri ya wilaya Kasulu ikiwemo jengo la utawala la ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji na wakuu wa idara sambamba na nyumba tano za watumishi wa idara ya afya.
(Picha na Fadhili Abdalla


Na Fadhili Abdallah,Kigoma
WITO umetolewa kwa Wakurugenzi wa halmashauri za Mkoa wa Kigoma kuwa wabunifu kwa kubuni na kutekeleza miradi yenye tija kwa jamii kww kutumia mapato yao ya ndani katika halmashauri zao.


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT),Jackson Mateso wakati wa ziara ya ukaguzi wa mradi wa Ujenzi wa nyumba tano za watumishi wa hospitali ya wilaya Kasulu ambazo zimejengwa kutokana na mapato ya ndani ya halmashauri hiyo ikiwa ni sehemu ya kikao cha ALAT mkoa.


Mateso alisema kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Kasulu,Joseph Kashushura ameonyesha kwa vitendo namna ambavyo halmashauri zinavyoweza kujibana kutumia rasilimali chache walizonazo katika kutekeleza miradi inayoleta tija kubwa kwa watumishi na jamii kwa jumla.


Katika ziara wajumbe wa ALAT mkoa Kigoma walitembelea mradi wa nyumba tazo za watumishi wa afya wa halmaahauri hiyo zilizojengwa kwa kutumia mapato ya ndani ambapo kiasi cha shilingi milioni 250 kimetumika kutekeleza mradi huo.


Kwa upande wake Katibu wa ALAT mkoa Kigoma, Zainabu Mbunda alisema kuwa ubuni na utekelezaji wa miradi umeonyesha mfano wa uongozi unaopaswa kuigwa ambao unatoa tija kubwa katika utendaji lakini pia kuleta maendeleo ya haraka kwa wananchi.


Mbunda ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Uvinza alisema wamejifunza jambo kubwa kupitia ziara hiyo na
Mkutano huo wa ALAT uliofanyika kwenye halmashauri ya wilaya Kasulu akiwa mwenyeji.


Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya Kasulu,Joseph Kashushura alisema ana mradi wa ujenzi wa jengo la utawala la halmashauri kwa ajili ya ofisi ya Mkurugenzi na wakuu wa idara lililopangiwa kutumia shilingi bilioni 3 lakini kutokana na kujibana na kutumia rasilimqli vizuri jengo hilo litakamilika kwa shilingi bilioni mbili likiwa ni jengo la ghorofa moja.


Kutokana na hali hiyo wameiomba TAMISEMI kuwapatia kiasi cha shilingi milioni 700 kati ya bilioni zilizobski kwenye mradi huo ili waweze kujenga ukumbi wa mikutano juu ya jengo hilo la ofisi na kwamba kufikia Juni mwaka ujao mradi huo utakuwa umekamilika ambapo kwa sasa umefikia asilimia 45.


Sambamba na hilo Mkurugenzi huyo alisema kuwa halmashauri inatekeleza mradi wa ujenzi wa nyumba tano za watumishi wa idara ya afya ili kuwezesha watumishi hao kuwa karibu na kituo cha utoaji huduma na kiasi cha shilingi milioni 250 zinatarajia kutumika kutoka mapato ya ndani ya halmashauri na mradi huo umefikia asilimia 80 ya utekelezaji.


Wajumbe wa kamati hiyo ya ALAT mkoa Kigoma akiwemo, Mathias Kigwinya Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Buhigwe alisema kuwa ujenzi wa nyumba hizo za watumishi wa afya unatoa morali kubwa kwa watumishi kuwa na uhakika wa mahali pa kuishi lakini unawahakikishia wananchi upatikanaji wa watoa huduma wakati wote.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) mkoa Kigoma, Jackson Mateso akiongoza wajumbe wa ALAT kukagua miradi ya ujenzi wa majengo ya utoaji huduma kwa wananchi kwenye halmashauri ya wilaya Kasulu ikiwemo jengo la utawala la ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji na wakuu wa idara sambamba na nyumba tano za watumishi wa idara ya afya.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments