RAIS SAMIA ATANGAZA BEI ZA MAFUTA KUSHUKA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Taifa tarehe 09 Mei, 2022 kuhusiana na suala la kupanda kwa bei ya Mafuta nchini akiwa Ikulu Jijini Dar es Salaam

Rais Samia amesema kwamba kuanzia Juni Mosi mwaka huu Watanzania wataanza kupata unafuu katika bei ya mafuta na kwamba kesho Mei 10 Waziri wa Nishati January Makamba, atazungumzia suala hilo bungeni jijini Dodoma.

"Nimeamua wananchi waanze kupata nafuu ya bei ya mafuta kuanzia Juni 1, 2022, nimeelekeza serikali tujibane na tujinyime ili kupata fedha kutoka katika matumizi ya kawaida ya serikali ili ziende kutoa nafuu katika bei za mafuta, kwenye kipindi kuelekea mwaka mpya wa fedha," amesema Rais Samia

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post