FILAMU YA THE ROYAL TOUR KUZINDULIWA JIJINI DODOMA...MTAKA KUIBUKA NA MAONESHO YA ZABIBU


Mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari leo Ofisini kuhusu mandalizi ya filamu ya Royal tour na kueleza umuhimu wa filamu hiyo kuwa ni fursa kiuchumi.


Na Dotto Kwilasa, DODOMA.

BAADA ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuzindua filamu ya The Royal Tour nchini Marekani na maeneo mengi nchini,Sasa filamu hiyo itazinduliwa Mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuitangaza na kuhamasisha utalii wa makao Makuu ya nchi.

Hatua hii imekuja siku chache baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka kutumia siku ya wafanyakazi -Mei Mosi kuomba kibali cha Rais Samia ili filamu hiyo izinduliwe mkoani Dodoma na kukubaliwa jambo linalotazamwa kutoa fursa mbalimbali za utalii na uwekezaji.

Akiongea na Waandishi wa habari ameeleza kuwa uzinduzi wa filamu hiyo utafanyika siku ya Jumapili tarehe 15/05/2022 kuanzia saa 12:00 Jioni katika Ukumbi wa mikutano wa JK Conversion Center huku akimtaja Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo.

Alifafanua kuwa uzinduzi huo utahusisha masuala mbalimbali ikiwemo maonyesho ya utamaduni na asili ya wenyeji wa mkoa wa Dodoma,mazao ya zabibu na ngoma za Kigogo na Kirangi.

"Maandalizi yamekamilika kutakuwa jogging na burudani itayobebwa na utamaduni wa Dodoma ngonga za kigogo na kirangi,milango iko wazi kwa watakaopenda kujiunga na tukio hili",alisema

Mkuu huyo wa mkoa wa Dodoma pia ametumia nàfasi hiyo kuzitaka sekta binafsi,wafanya biashara na Wadau wa maendeleo kushiriki kwenye tuki hilo ili kukuza sekta ya utaalii na kufungua mipango ya sekta ya uchumi

Aliongeza kuwa"zao la zabibu linaongeza thamani yake kutoka kwenye wine kwenye mvinyo, tutakuwa na maonyesho ya mazao ya zabibu ,"alisema

Alisema kuwa Ofisi yake imetoa fursa kwa baadhi ya Wilaya kuangalia tukio hili kupitia vyombo vya habari na utaratibu wote umekamilika.

Ikumbukwe kuwa mbali na Dodoma filamu ya The Royal Tour ilianza kuzinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huko nchini Marekani na hatimae jijini Arusha ,Zanzibar na Dar es Salaam.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments